STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, August 14, 2014

CAS kuamua hatma ya Suarez leo

MAHAKAMA ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) imethibitisha kwamba itatangaza maamuzi yake katika kesi ya kufungiwa kwa Luis Suarez leo.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uruguay alifungiwa kujihusisha na masuala yote ya soka kwa miezi minne kufuatia kumng'ata beki wa ti,u ya taifa ya Italia, Giorgio Chiellini wakati wa mechi yao ya Kombe la Dunia mjini Natal, Juni.
Chama cha soka cha nchi yake haraka kilipinga adhabu hiyo, lakini FIFA ilikataa kupunguza adhabu hiyo na kusababisha kesi hiyo kupelekwa CAS.
Suarez kisha akahama Liverpool na kutua Barcelona, ambao wamerudia mara kwa mara kuelezea matumaini yao kwamba atacheza mepema kuliko ilivyotarajiwa awali.
Na sasa imethibitishwa kwamba hatima yake itajulikana saa 10:00 leo, baada ya rufaa yake kusiklizwa.
"Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) itatangaza maamuzi yake katika suala la Luis Suarez, FC Barcelona na chama cha soka cha Uruguayan Alhamisi Agosti 14, 2014 majira ya saa 4:00 jioni," taarifa rasmi ilisomeka.
"Kesi hii ilisikilizwa Agosti 8, 2014 katika ofisi za CAS mjini Lausanne. Kwa maombi ya warufani na kwa maafikiano na Fifa, CAS ilifanya hatua zake za usuhilishi.
"Kufuati hilo, Jopo la CAS liliafiki kutoa maamuzi yake ndani ya muda mfupi lakini kwa mazingira yanayofuata baadaye."

No comments:

Post a Comment