STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, August 28, 2014

Kocha Mexime awakuna wachezaji Mtibwa Sugar

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjVzufGN29F3EQO9M7DaKGF8TdIspdiztoQgVTGD8zWO2W1YB8ab9wJMCTc5-pqvYnHKlB2JLmq-wB7XAxld2-4Kh7Xb9sz0CVRFZKAKfjnWABu_wB-VYdQ1hq18g8-TqWULxVQIjQbjic/s1600/IMG_0621.JPG
Benchi la ufundi la Mtibwa Sugar
MSHAMBULIAJI nyota wa Mtibwa Sugar, Abdallah Juma amemwagia sifa kocha wake, Mecky Mexime huku akiitabiria Mtibwa kufanya vema kwenye msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Abdallah maarufu kama 'AJ' aliyeifungia Mtibwa mabao manne msimu uliopita ikiwamo hat trick wakati wakiizamisha JKT Oljoro, alisema tangu kocha wao amerejee toka masomoni amekuwa akiwapa mbinu ambazo zinawafanya kuzidi kuwa wakali na kufufua ari zao.
Nyota huyo wa zamani wa AFC Arusha, Kagera Sugar na Simba, alisema kwa namna kocha wao anavyowapa mbinu za kinazohusu mikasa aliyokutana nayo katika maisha yake.
"Kocha wetu ni kama 'amezaliwa' upya, yupo tofauti na msimu uliopita kwa jinsi anavyotupa mbinu mpya ambazo tunaamini zitaifanya Mtibwa Sugar itishe kwenye ligi ya msimu huu," alisema.
Abdallah alisema mpaka Septemba 20 ligi itakapoanza kwa wao kuwakaribisha Yanga kwenye uwanja wa Jamhuri watakuwa wameiva na kuanza mbio zao za kurejesha heshima yao baada ya kushindwa kufanya vema ligi iliyopita.
Mshambuliaji huyo alisema anaamini msimu wa 2014-2015 utakuwa wa Mtibwa Sugar licha ya kwamba wadau wa soka wanaziangalia Simba, Yanga, Azam na pengine Mbeya City baada ya msimu uliopita kupanda Ligi Kuu na kuonyesha kiwango cha hali ya juu.

No comments:

Post a Comment