Twiga Stars kwenda Bondeni kirafiki
KIKOSI cha timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) inatarajia kuondoka nchini Ijumaa
(Agosti 29 mwaka huu) kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya mechi ya
kirafiki na timu ya Taifa ya nchi hiyo (Banyana Banyana).
Twiga
Stars inakwenda huko kwa mwaliko wa Chama cha Mpira wa Miguu Afrika
Kusini (SAFA) kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa Jumapili (Agosti 31
mwaka huu) katika mji wa Polokwane.
Msafara
wa timu hiyo utaongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Saloum ambapo utajumuisha wachezaji 18
na benchi la ufundi lenye watu watano.
Wachezaji
kwenye msafara huo ni Amina Bilali, Anastaz Katunzi, Asha Rashid,
Donisia Minja, Esther Chabruma, Etoe Mlenzi, Fatuma Jawadu, Fatuma
Makusanya, Fatuma Maonya, Fatuma Swaleh, Happiness Mwaipaja, Maimuna
Said, Mwajuma Abdillahi, Mwanahamis Shurua, Shelda Mafuru, Sophia
Mwasikili, Therese Yona na Zena Rashid.
Benchi
la Ufundi linaongozwa na Kocha Rogasian Kaijage, na msaidizi wake Nasra
Mohamed. Wengine ni Christine Luambano (daktari), Furaha Mnele (Meneja)
na Mwanahamisi Nyomi (mtunza vifaa). Timu hiyo inatarajia kurejea
nchini Septemba 2 mwaka huu kwa ndege ya Fastjet.
No comments:
Post a Comment