CHAMA cha Soka nchini
Misri kiomeongeza idadi ya nchi zinazowania uaandaaji wa Fainali za Afrika 2017 baada ya kujitosa kwenye kinyang'anyiro hicho ambacho Tanzania nacho imeingia tangu juzi.
Misiri ilianda mara ya mwisho fainali hizo mwaka 2006 na inawania nafasi hiyo na nchi nyingine baada ya waliokuwa wawe wenyeji, Libya kutangaza kujitoa.
Vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoendelea
nchini Libya viwalazimisha kujitoa kwa mara ya pili baada ya mwaka jana kushindwa na kuiachia Afrika Kusini kuandaa.
Kutokana na hali hiyo ambayo imeikwaza nchi hiyo kutekeleza mikakati ya ujenzi wa viwanja
na kuifanya Shirikisho la Soka Barani Afrika-CAF kutafuta
mwenyeji mwingine wa michuano hiyo.
Chanzo kimoja cha habari kutoka
ndani ya EFA kimebainisha nia ya kutaka kuwa mwenyeji wa michuano hiyo
lakini bado hawajafanya uamuzi wa mwisho kuhusiana na suala hilo.
Makamu
wa rais wa EFA Hassan Farid naye alithibitisha nia yao hiyo lakini
amesema bado wanataka kuzungumza na baadhi ya wizara serikalini ili
kupata ushirikiano wao.
Misri ni mojawpao ya nchi chake barani Afrika
zenye miundo mbinu mizuri ya kuandaa michuano mikubwa kama Afcon.
No comments:
Post a Comment