UHONDO zaidi umezidi kuongezwa kwenye maandalizi ya Tamasha la Miaka 16 ya Kituo cha Mazoezi cha Home Gym baada ya waratibu wake kuongeza vikundi vya Ngoma Asilia.
Vikundi mbalimbali vya ngoma asilia toka Mbagala jijini Dar es Salaam na burudani ya muziki wa kizazi kipya vinatarajiwa kutumbuiza kwenye tamasha hilo litakalofanyika Sept. 6.
Tamasha hilo litafanyika kwenye uwanja wa Mwenge likijumuisha michezo mbalimbali ikiwamo ya soka kwa timu za maveterani, Jogging na watunisha misuli.
Akizungumza na Blogu hii, mratibu wa tamasha hilo, Andrew Mangomango alisema vikundi hivyo vya ngoma asilia vinatokea Mbagala na vitatumbuiza kabla ya wakati wa michezo ya tamasha lao la kuadhimisha miaka 16 ya Home Gym.
Mangomango alisema mpaka sasa wamefanikiwa kusajili klabu 12 za maveterani, klabu zaidi ya 20 za Jogging na wanamichezo mbalimbali wa kutunisha misuli, kunyanyua vitu vizito, mieleka na mabondia kwa ajili ya shoo la tamasha hilo.
Alisema kuwa tayari wadhamini mbalimbali wameanza kujitokeza kuwapiga tafu ikiwamo kampuni ya General Shami Investment Co. Ltd na wengine.
Mangomango alisema mbali na burudani na muziki na shoo za wanamichezo pia, siku hiyo wanamichezo mbalimbali watachuana katika kuvuta kamba, kukimbiza kuku na kukimbia kwenye magunia na washindi watapewa zawadi mbalimbali.
No comments:
Post a Comment