STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, August 17, 2014

Van Gaal aanza kwa kichapo nyumbani EPL


KOCHA mpya wa Manchester United , Mholanzi, Louis van Gaal amekaribishwa na kipigo cha mabao 2-1 katika mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu dhidi ya Swansea City ndani ya dimba la Old Trafford.
Hii ni mara ya kwanza kwa Man United kupoteza mechi ya ufunguzi wa msimu katika uwanja wake wa Old Trafford.
Swansea City walikuwa wa kwanza kuandika bao la kuongoza katika dakika ya 28 kupitia kwa Ki Sung-yueng.
Mshambuliaji na nahodha wa Man United, Wayne Mark Rooney aliisawazishia timu yake bao hilo katika dakika ya 53 baada ya kupiga tikitaka mpira wa kona uliochongwa na Juan Mata.
Gylfi Sigurdsson ndiye aliibuka shujaa wa kuifungia bao la ushindi Swansea katika dakika ya 72 na kukalia usukani wa ligi kuu kwa saa kadhaa.
Baada ya kumalizika kwa mechi hiyo pointi za muhimu alizozungumza Van Gaal ni:
-Sio kwamba safu ya ulinzi ndio inatakiwa kuboreshwa bali ni timu nzima.
-Amesema hatapaniki kwasababu ya Man United kupoteza.
-Atawapa nafasi zaidi wachezaji kumpatia ushindi.
Kikosi cha Manchester United: De Gea, Jones, Smalling, Blackett, Lingard (Januzaj), Fletcher, Herrera, Young, Mata, Rooney (c), Hernandez (Nani)
Wachezaji wa akiba: Amos, James, M Keane, Fellaini, Kagawa
Kikosi cha Swansea: Fabiański; Rangel, Williams, Amat, Taylor, Ki, Shelvey, Dyer, Sigurðsson, Routledge, Bony (Gomis)
Wachezaji wa akiba: Tremmel, Bartley, Richards, Tiendalli, Montero, Sheehan.

No comments:

Post a Comment