KOCHA mpya wa timu ya
taifa ya Brazil, Dunga amemuita mshambuliaji wa zamani wa vilabu vya
Real Madrid, Manchester City na AC Milan, Robinho kuziba pengo la
majeruhi Hulk wa Zenith kwa ajili ya mechi mbili za kimataifa za kirafiki dhidi ya
Colombia na Ecuador.
Dunga ambaye alitaja kikosi chake cha kwanza toka
achukue mikoba kwa mara ya pili kutoka kwa Luiz Felipe Scolari baada ya
Kombe la Dunia, amemchukua nyota huyo mwenye umri wa miaka 30 ambaye
ameichezea nchi hiyo mechi 92.
Robinho amerejea nyumbani Brazil kucheza
katika klabu ya Santos ambayo ndio alianzia kucheza soka lake baada ya
AC Milan kumuuza kwa mkopo wa mwaka mmoja.
Dunga aliyewahi kuinoa
Brazil katika miochuano ya Kombe la Dunia mwaka 2010 kabla ya kutimuliwa
sasa anaelekea katika mchezo dhidi ya Colombia utakaochezwa jijini
Miami Ijumaa hii akiwa na wachezaji 10 pekee waliokuwepo katika kikosi
cha Scolari.
Baada ya kukwaana na Colombia, Brazil itachuana na Ecuador
huko East Rutherford jijini New Jersey Septemba 9 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment