Evodius Mtawala (kulia) akiwa na viongozi wenzake wa TFF kabla ya kubwanga manyang'a |
TAARIFA zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa, aliyekuwaMkurugenzi wa wa Vyama na Masuala ya Kisheria
katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Evodius Mtawala, ameachia
ngazi katika nafasi hiyo.
Mtawala Katibu Mkuu huyo wa zamani wa Simba, alikuwa na hali ya kutokuelewana na uongozi wa shirikisho hilo
na ndiyo chanzo cha kung'atuka TFF.
Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa, alithibitisha
kuachia ngazi kwa Mtawala lakini akasema ni kutokana na sababu mbalimbali za
taaluma yake ya uanasheria.
“Ni kweli Mtawala hataendelea kufanya kazi TFF
lakini ameamua kuchia ngazi mwenyewe kutokana na sababu mbalimbali alizodai
kwamba ni kujikita na taaluma yake zaidi kwa sasa, lakini mambo mengine juu ya
hilo yatabaki kuwa siri baina yake na mwajiri wake.
“Ila mpaka makubaliano ya mwisho yalieleza
kuwa itakapofika mwisho wa mwezi wa nane (jana 31, Agosti) atakuwa tayari
ameshakabidhi ofisi na kuendelea na masuala ambayo alidai anahitaji kujikita
zaidi kulingana na taaluma yake,” alisema Mwesigwa.
No comments:
Post a Comment