Watatu
hao waliichezea Ujerumani katika fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2014
dhidi ya Argentina kabla ya kuamua kustaafu soka ya kimataifa.
Klose,
ambaye ni mfungaji bora wa kihistoria wa Ujerumani kwa mabao yake 71,
ametungika daluga baada ya kuwa mfungaji wa mabao mengi zaidi katika
historia ya Kombe la Dunia.Hata hivyo furaha yao ya kupokea tuzo hizo ziliingia shubiri baada ya kuishuhudia Ujerumani ikifa mbele ya Argentina.
Winga mpya wa Manchester United, Angel di Maria ametengeneza mabao matatu na kufunga moja katika mchezo huo uliochezwa mjini Dusseldorf, Ujerumani.
Mchezaji
huyo ghali zaidi kusajiliwa Manchester United na Uingereza nzima
alipika mabao ya Sergio Aguero, Erik Lamela na Federico Fernandez kabla
ya kufunga na lake mwenyewe siku 52 tangu bao la Mario Gotze katika
muda wa nyongeza liipe Ujerumani ubingwa wa dunia nchini Brazil.
Ujerumani walipata mabao yao kupitia Andre Schurrle Gotze aliyefunga la pili kwa mabingwa hao wa dunia.
No comments:
Post a Comment