Baba na mwana |
WAKATI baba yake Radamel Garcia, akibainisha kuwa Arsenal, Liverpool, Manchester City na Juventus, zilikuwa zikipigana mkumbo kumsajili kabla ya kuhamia Manchester United, mshambuliaji nyota wa Colombia aliyekuwa As Monaco ya Ufaransa, Radamel Falcao amebainisha kuwa ametimiza ndoto zake baada ya kukamalisha usajili wa mkopo kwenda kwa Mashetani Wekundu. Falcao aliiambia runinga ya Manchester Utd, MUTV kuwa alikuwa na ndoto za siku nyingi kukipiga katika Ligi Kuu nchini Uingereza kutokana na ushindani uliopo.
Nyota huyo aliendelea kudai kuwa ametua katika klabu ambayo ni bora kabisa nchini humo na sasa kila kitu kinakwenda sawa.
Falcao, 28 alisafiri kwenda jijini Manchester kwa ajili ya vipimo vya afya Jumatatu jioni huku United wakithibitisha dili hilo baada ya kupita saa mbili na nusu toka dirisha la usajili lifungwe.
United wameilipa Monaco kitita cha paundi milioni sita ili kupata huduma ya Falcao kwa msimu mmoja huku wakiwa na chaguo la kumsajili moja kwa moja wakitoa kitita kingine cha euro milioni 55.
Hata hivyo baba yake mzazi amebainisha kabla ya kutua Old Trafford, Falcao alikuwa akiwindwa na klabu nne tofauti zikiwamo tatu za England ili kunasa saini yake kabla mshambuliaji huyo hajaamua kutuma Manchester United kwa mkopo akitokea Monaco.
Mzee huyo Ramadel Garcia alinukuliwa na The Mirror kuwa alisema Real Madrid waliamua kutomfuatilia Falcao, tofauti na Juventus, Arsenal, Manchester City na Liverpool.
No comments:
Post a Comment