MICHUANO ya Ligi Daraja la Pili (SDL) inayoshirikisha timu 24 zitakazocheza katika
makundi manne ya timu sita sita kwa mtindo wa nyumbani na ugenini itaanza
kutimua vumbi Novemba 22 mwaka huu.
Kamati
ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyoketi jijini
Dar es Salaam jana (Oktoba 29 mwaka huu) chini ya Mwenyekiti wake Geofrey
Nyange ilipitia maandalizi maandalizi ya ligi hiyo ikiwemo mwongozo wake
(roadmap).
Kwa
mujibu wa mwongozo huo, usajili wa wachezaji utamalizika Oktoba 31 mwaka huu.
Kipindi cha pingamizi ni kuanzia Novemba 1 hadi 7 mwaka huu wakati Kamati ya
Sheria na Hadhi za Wachezaji inatarajia kukutana Novemba 11 mwaka huu kwa ajili
ya kupitisha usajili.
Pia
Kamati ya Mashindano imepitisha viwanja vya timu zote, isipokuwa uwanja wa timu
ya Mpanda United ya Katavi na ule wa Town Small Boys ya Tunduru mkoani Ruvuma.
Uwanja
wa Town Small Boys haukupitishwa kwa vile hauna uzio wa kudumu ( wa chuma) wa
kutenganisha wachezaji na washabiki, na pia ufikaji wa timu Tunduru ni mgumu
kutokana na ubovu wa barabara ikizingatiwa kuwa ligi hiyo itachezwa hadi
kipindi cha Masika.
Kwa
upande wa uwanja wa Mpanda United, umekataliwa kwa vile hauna vigezo vya msingi
vinavyotakiwa ikiwemo vyumba vya kubadilishia nguo, kutokuwa na nyasi na uzio
wa kudumu kutenganisha wachezaji na washabiki.
No comments:
Post a Comment