Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Ahmed Kipozi ( pili kulia mbele) akiwa na baadhi ya viongozi wa Chalinze mara baada ya sherehe za MHCS Ltd |
Mrajisi wa Vyama vya Ushirika, Dk Audax Rutabazibwa akipata maelezo toka kwa Marieta Urassa baada ya kumkabidhi kiwanja eneo la Kibiki |
Mzee eneo letu ni kuanzia hapa mpaka kule... |
Mmoja wanachama wa MHCS Ltd Seleka Sanga (wa pili kulia) akikabidhiwa eneo lake Kibiki |
Marieta Urassa akipongezwa na Mrajisi wa vyama mara baada ya kukabidhiwa eneo lake jana |
Wachekeshaji Eric Ivyo ivyo na Mkono wa Mkonole nao walikuwa mashuhuda wa shughuli za wanachama wa MHCS walipokabidhiwa viwanja vyao |
Viongozi wa MHCS Ltd wakiwa katika picha ya pamoja na wageni wa shughuli zao, DC Kipozi, Mrajisi Dk Rutabazibwa na Diwani wa Bwilingu, Hemed Karama Nassa (mbele). |
Sehemu ya wanachama wa MHCS Ltd wakiwa kwenye sherehe hizo kabla ya kukabidhiwa viwanja vyao |
Mjumbe wa Bodi ya Uongozi wa MHCS, Hellen Khamsini akisoma risala ya chama chao mbele ya meza kuu |
Mradi huo ambao umeanza kwa MHCS kugawa viwanja kwa wanachama 40 jana kijijini hapo, unatarajiwa kuanza mapema mwakani ambapo utawawezesha wanachama wao kumudu kulipia kidogo kidogo gharama za nyumba hizo.
Uongozi wa MHCS kupitia risala yao iliyosomwa mbele ya mgeni rasmi wa sherehe za uzinduzi wa ofisi ya chama hicho eneo la Kibiki-Chalinze pamoja na ugawaji wa viwanja na vyeti vya hisa kwa wanachama wao, umesema tumaini lao ni kuhakikisha kila mwanachama wao anakuwa na makazi bora na ya kisasa kama njia ya kutekeleza malengo ya waasisi wa chama hicho kilichoanzishwa mwaka 1971.
Risala hiyo iliyosomwa na Mjumbe wa Bodi ya Uongozi wa MHCS Ltd, Hellen Khamsini, ilisomwa mbele ya Kaimu Mrajisi wa Vyama vya Ushirika nchini, Dk Audax Rutabazibwa na kudai kuwa awamu ya kwanza ya kupata ardhi ulihusisha ekari 45 ambalo limetoa jumla ya viwanjan93 vikiwamo viwanja vya makazi na huduma za jamii kama misikiti, makanisa na viwanja vya kuwekeza.
"Katika awamu ya pili tulipata eneo la ukubwa wa ekari 177 lililotoa viwanja 374 kati ya hivyo viwanja 278 vimegawiwa kwa wanachama na vilivyobaki ambavyo ni 96 vinabaki kuwa mali ya chama ambavyo vinahusisha makazi, huduma ya kijamii kama masuala ya dini, michezo na eneo la uwekezaji ambapo tuna nia ya kujenga hoteli kubwa ya kisasa ya hadhi ya Nyota Tano."
Uongozi wa chama hicho umesema kuwa matarajio yao mara baada ya kuanza kujenga mradi huo wa nyumba za kisasa kwa wanachama wao katika eneo hilo la Kibiki, wamepanga kupata maeneo zaidi ya ardhi katika mikoa saba ya Arusha, Diodoma, Mwanza, Mbeya, Mtwara, Morogoro na Lindi kabla ya kuyaangalia maeneo mengine lengo likiwa kupanua wigo mpana wa chama chao na kusaidia kusambaza maendeleo ya makazi kwa watanzania wote bila kujali jinsia, dini, rangi au kabila.
Hata hivyo chama hicho kilisema kuwa kimekuwa kikikumbana na changamoto mbalimbali na kuuomba uongozi wa wilaya ya Bagamoyo na serikali kwa ujumla kuwasaidia kuwatatuloia baadhi ya kero kama miundo mbinu ya barabara, huduma za maji, umeme na mfumo wa maji taka katika maeneo wanayoyamiliki kwa sasa ili kuwapa unafuu wanachama wao.
Aliyekuwa mgeni rasmi wa hafla hiyo, Dk Rutabazibwa alisema ofisi yake ipo bega kwa bega na MHCS na kuahidi kufuatilia kuona mradi wanaotarajiwa kuufanya unafanikisha na kuwasaidia wanachama wao kupata nyumba wanazomudu kulizipa.
Naye Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Ahmed Kipozi alisema ofisi yake imeupokea mradi huo wa nyumba za kisasa na bora za bei nafuu wilayani mwake, na kuahidi kuwa bega kwa bega na uongozi wa chama hicho huku akiwasisitizia kutowatenga wakazi wenyeji katika mradi huo ili kujijengea mazingira mazuri ya kufanikisha sambamba na kujenga umoja na mshikamano baina yao.
Baadhi ya wanachama wa chama hicho, Hellen Khamsini, Zahir Mshana na Dionis Moshi walisema wamenufaika mno na chama chao katika kupata makazi ambayo hawakutarajia na kufurahia kuanzishwa kwa mradi mpya eneo la Kibiki wakiamini litazidi kupanua wigo wa kuishi kisasa kwa sababu eneo lao la sasa la Mwenge ni dogo na nyumba zake kwa sasa zinaonekana kama gofu kwa kuchakaa.
"Kwa kweli nashukuru tangu niwe mwanachama nikijiunga mwaka 1972 nimenufaika kwa mengi na kwa mara ya kwanza nimeweza kupata mahali pa kuishi na sasa kumiliki kiwanja eneo la Kibiki, matarajio yangu kuzidi kuendelea kunufaika hata kwa vizazi vyangu vijavyo," alisema Mushi.
Mshana alisema anaamini mradi mpya utamfaa zaidi kwa sababu familia yake imepanuka akiwa na wajukuu na eneo analoishi kwa sasa Mwenge jiji ni dogo hivyo anaushuruku uongozi kwa juhudi wanazofanya, licha ya kukiri mwanzoni chama chao kilionekana kikienda sivyo kutokana na ubadhilifu uliofanywa na viongozi waliopita ambao walitimuliwa na kuweka wapya wanaowaletea maendeleo sasa.
Chama hicho kilichoasisi wa Rais wa Kwanza wa Tanzania, Mwalimu Nyerere na aliyekuwa Waziri Mkuu, Rashid Kawawa na waliokuwa mawaziri wa awamu ya kwanza, Dereck Brayson na John Mhaville kikiwa na wanachama 25, lakini mpaka sasa ina jumla ya wanachama 385.
No comments:
Post a Comment