Jamani msiniangushe kwa Mtibwa si mmesikia wanene walivyosema? Kocha Patrick Phiri akiteta na wachezaji wake katika moja ya mazoezi ya timu hiyo |
Vita ya Kagera na Yanga kama hii itakuwa kesho Kaitaba |
Azam wameifuata Ndanda wakiugulia kipigoi cha JKT Ruvu. Watapona Nangwanda Sijaona? |
Pambano hilo litakalochezwa uwanja wa Jamhuri, Morogoro ni miongoni mwa mechi sita zitakazochezwa siku ya kesho kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.
Simba kupitia uongozi wake ulitangaza kumpa kocha wao mechi mbili dhidi ya Mtibwa na ile itakayofuata wikiendi ijayo dhidi ya Ruvu Shooting kama kipimo cha mwisho cha kumvumilia kutokana na matokeo mabaya inayopata timu yao msimu huu.
Katika mechi tano za awali Simba imeambulia sare huku relodi ikionyesha haijaonja ushindi wa aina yoyote katika jumla ya mechi 11 za Ligi tangu walipoiotea Ruvu Shooting kwa kuilaza mabao 3-2.
Baadhoi ya wadau wa soka wamekuwa wakiushutumu uongozi wa Simba kwa maamuzi hayo ya kumbana Phiri wakati ikijua hakuhusika na usajili wa wachezaji waliopo kikosi kwa sasa Msimbazi.
Hata hivyo Mtibwa kupitia Msemaji wake, Thobias KIfaru amesema kuwa Simba wasitarajie mteremko kwao kwani wamejipanga kuwalipua ili kurahisisha kazi ya kumtimua kocha wao.
Ukiacha mechi hiyo, kesho pia kutakuwa na mechi ya kukata na shoka kati ya Yanga itakayokuwa wageni wa Kagera Sugar uwanja wa Kaitaba, huku watetezi Azam wakiwafuata Ndanda Fc iliyomtimua kocha wao, Dennis Kitambi.
Mechi nyingine za kesho ni pamoja na maafande wa JKT Ruvu watakaowakaribisha maafande wa Polisi Moro ambao wanauguza kipigo cha 1-0 walichopewa na Ruvu Shooting wikiendi iliyopita.
Pia kesdho kutakuwa na pambano kati ya Coastal Union watakaokuwa wenyeji wa Ruvu Shooting na Stand United kuikaribisha PRisons-Mbeya na siku ya Jujmapili kutakuwa na pambano moja tu kati ya Mgambo JKT itakayoialika Mbeya City uwanja wa Mkwakwani.
Yanga ambayo inatokea Shinyanga ilipoilipua Stand united kwa mabao 3-0 tayari ipo mjini Kagera tayari kwa pambano hilo na msemaji wao, Baraka Kizuguto ameweka bayana kwamba wamezifuata pointi tatu Kaitaba.
Katika mechi yao ya msimu uliopita kwenye uwanja huo Yanga iliwatambia wenyeji wao kwa bao 2-1, jambo ambalo Kizuguto anaamini kitaendelezwa tena kesho.
Mpaka sasa Ligi hiyo inaoongozwa na Mtibwa yenye pointi 13 ikifuatiwa na watetezi Azam wenye pointi 10 sawa na Yanga ila zikitofautiana mabao ya kufunga na kufungwa kisha Coastal Union, JKT Ruvu na Ruvu Shootying, Simba a.k.a Wazee wa Sare wenyewe wanashika nafasi ya 10 wakiwa na pointi 5.
No comments:
Post a Comment