MAKOCHA
35 wameteuliwa kushiriki kozi ya ukocha ya Leseni C ya Shirikisho la
Mpira wa Miguu Afrika (CAF) itakayofanyika mjini Morogoro kuanzia
Novemba 5 hadi 19 mwaka huu.
Kozi
hiyo itaendeshwa na Mkufunzi wa CAF, Sunday Kayuni na itafanyikia
Mchikichini College ambapo washiriki wote wanatakiwa kuwasilisha vyeti
vyao vya ukocha vya ngazi ya Kati (Intermediate) pamoja na vyeti vya
kitaaluma vya elimu ya sekondari (academic).
Washiriki
wa kozi hiyo ni Abdulmaliki Nemes (Airport FC), Ahmed Haule
(Kilimanjaro Talented Youth Sports Centre), Ally Jangalu (Moro Kids),
Amri Saidi (Mwadui FC) na Athuman Kambi (Morogoro).
Wengine ni Charles Mwakambaya
(Burkina Faso FC), Damian Mussa (Alliance One) na Daudi Sichinga (Kasulu
United), Denis
Maneva (Shule ya Msingi Logo), Edgar Juvenary (JUT- Mlale) na Hamisi
Mangolosho (Shule ya Msingi Mtimbwilimbwili).
Pia wamo Henry Ngondo (Chalinze
Academy), Issa Hamisi (Polisi Kilimanjaro), Jumanne Chale (Dar es
Salaam), Kizito Mbano (Masasi Alliance), Martin Saanya (Magereza
Morogoro) na Masoud Gumbwa (Sokoine University Academy).
Wengine ni
Mbwana
Makata (Oljoro JKT), Mrage Kabange (Kagera Sugar), Muhibu Muhibu (Stand
United FC), Nsubuga Solomon (Kishoto FC), Nyamtimba Muga (Kizuka
Secondary), Oscar Mirambo (Makongo), Rashid Abdallah (Tech Fort
Academy), Renatus Shija (Rhino Rangers), Safari Nyerere (Elimu Sports
Academy) na Said Lyakuka (Kizuka Stars).
Simeon
Mwesa (Mtibwa Sugar U20), Simon Shija (Tabora), Suleiman Mtungwe (Ruvu
Shooting), Swalehe Allawi Abdul (Alliance Academy), Yasin Bashiri (Kick
Off Sports Academy) na Zuberi Katwila (Mtibwa Sugar).
Wakati
huo huo, kutakuwa na kozi ya wiki mbili ya ukocha ya ngazi ya Kati
(Intermediate) itakayofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Desemba 29
mwaka huu.
Makocha wote wanaotaka kushiriki kozi hiyo wanatakiwa kutuma maombi katika Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA).
No comments:
Post a Comment