Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete akizungumza na Dkt.Edward Shaeffer wa hospitali ya Johns
Hopkins (kushoto) na Daktari wa Rais Profesa Mohamed Janabi (kulia)
muda mfupi baada ya kuwasili ili kufanyiwa upasuaji katika Hospitali ya
Johns Hopkins iliyopo Baltimore Maryland Marekani Jumamosi
asubuhi.Upasuaji huo uliochukua muda wa saa moja na nusu ulifanyika
salama.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na daktari Bingwa Mpasuaji
Edward Shaeffer muda mfupi kabla ya kuingia kwenye chumba cha upasuaji
uliofanyika katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyopo Baltimore
Maryland nchini Marekani Jumamosi asubuhi(picha na Freddy Maro)
======= ====== ======
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete alfajiri ya jana, Jumamosi, Novemba 8, 2014, alifanyiwa
upasuaji wa tezi dume (prostrate) katika Hospitali ya Johns Hopkins
iliyoko Baltimore, Jimbo la Maryland, Marekani.
Rais Kikwete amefanyiwa upasuaji huo baada ya madaktari waliomfanyia
uchunguzi wa afya yake kujiridhisha kuwa Rais alikuwa anahitaji
matibabu ya aina hiyo.
Upasuaji huo uliofanyika alfajiri na kuchukua kiasi cha saa moja
unusu, umefanyika salama na kwa mafanikio makubwa. Hali ya Mheshimiwa Rais Kikwete inaendelea vizuri, bado yuko wodini akiendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari na kupatiwa tiba.
Wananchi wataendelea kupewa taarifa sahihi kuhusu hali ya Rais Kikwete
kwa kadri zitakavyokuwa zinapatikana.
Imetolewa na
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS, IKULU
DAR ES SALAAM,
NOVEMBA 9, 2014

No comments:
Post a Comment