Senzo Meyiwa enzi za uhai wake |
Yaya Toure kutetea tena tuzo yake ya Mwanasoka Bora Afrika |
Jina la kipa huyo aliyekuwa na miaka 27 ni miongoni mwa orodha ya wanasoka walioteuliwa na Shirikisho la Soka Brani Afrika, CAF iliyotangazwa kwa ajili ya tuzo za Mwanasoka Bora Afrika na wale wanaocheza nyumbani kwa mwaka 2014.
Iwapo ataibuka kidedea ataweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza Marehemu kushinda tuzo hiyo.
Katika orodha ya Mwanasoka Bora Afrika, mtetezi Yaya Toure ameteuliwa tena kuwania tuzo hiyo akichuana na wakali kama Emmanuel Adebayor wa Togo, Ahmed Musa wa Nigeria na Kwado Asamoah wa Ghana, huku Mbwana Samatta aliyekuwa kwenye orodha ya mwaka jana akipigwa chini safari hii.
Jumla ya wachezaji 25 wameingia kwenye kinyang'anyiro cha tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika, wakati wengine 20 watawania tuzo ya Mchezaji anayecheza Afrika.
Washindi wa vipengele hivyo viwili watapatikana baada ya kura zitakazopigwa na Makocha Wakuu na Wakurugenzi wa Ufundi wa vyama vya soka na Mashirikisho wanachama wa CAF.
Sherehe za tuzo zitafanyika Alhamisi ya Januari 8, mwakani mjini Lagos, Nigeria. Yaya Toure ndiye anashikilia tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika, wakati Mohamed Aboutreika wa Misri anashikilia tuzo ya Mwanasoka Bora Anayecheza Afrika ambaye hata hivtyo safari hii hayupo.
Orodha kamili ya Wanasoka walioteuliwa kuwania tuzo hizo mwaka huu ni kama ifuatavyo;
TUZO YA MWANASOKA BORA AFRIKA1. Ahmed Musa (Nigeria, CSKA Moscow)
2. Asamoah Gyan (Ghana, Al Ain)
3. Dame N’doye (Senegal, Lokomotiv Moscow)
4. Emmanuel Adebayor (Togo, Tottenham)
5. Eric Maxim Choupo-Moting (Cameroon, Schalke)
6. Fakhreddine Ben Youssef (Tunisia, CS Sfaxien)
7. Ferdjani Sassi (Tunisia, CS Sfaxien)
8. Yao Gervais ‘Gervinho’ (Ivory Coast, Roma)
9. Islam Slimani (Algeria, Sporting Lisbon)
10. Kwadwo Asamoah (Ghana, Juventus)
11. Mehdi Benatia (Morocco, Bayern Munich)
12. Mohamed El Neny (Misri, Basel)
13. Pierre-Emerick Aubameyang(Gabon,B. Dortmund)
14. Raïs M'Bolhi (Algeria, Philadelphia Union)
15. Sadio Mané (Senegal, Southampton)
16. Seydou Kieta (Mali, As Roma)
17. Sofiane Feghouli (Algeria, Valencia)
18. Stephane Mbia (Cameroon, Sevilla)
19. Thulani Serero (Afrika Kusini, Ajax)
20. Vincent Aboubakar (Cameroon, Porto)
21. Vincent Enyeama (Nigeria, Lille)
22. Wilfried Bony (Ivory Coast, Swansea)
23. Yacine Brahimi (Algeria, Porto)
24. Yannick Bolasie (DRC, Crystal Palace)
25. Yaya Toure (Ivory Coast, Man City)
TUZO YA MWANASOKA BORA ANAYECHEZA AFRIKA
1. Amr Gamal (Misri, Al Ahly)
2. Abdelrahman Fetori (Libya, Ahly Benghazi)
3. Bernard Parker (Afrika Kusini, Kaizer Chiefs)
4. Bongani Ndulula (Afrika Kusini, Amazulu)
5. Akram Djahnit (Algeria, ES Setif)
6. Ejike Uzoenyi (Nigeria, Enugu Rangers)
7. El Hedi Belamieri (Algeria, ES Setif)
8. Fakhereddine Ben Youssef (Tunisia, CS Sfaxien)
9. Ferdjani Sassi (Tunisia, CS Sfaxien)
10. Firmin Mubel Ndombe (DRC, AS Vita)
11. Geoffrey Massa (Uganda, Pretoria University)
12. Jean Kasusula (DRC, TP Mazembe)
13. Kader Bidimbou (Kongo, AC Leopards)
14. Lema Mabidi (DRC, As Vita)
15. Mudathir Al Taieb (Sudan, Al Hilal)
16. Roger Assalé (Ivory Coast, Sewe Sport)
17. Senzo Meyiwa (Afrika Kusini, Orlando Pirates)
18. Solomon Asante (Ghana, TP Mazembe)
19. Souleymane Moussa (Cameroon, Coton Sport)
20. Yunus Sentamu (Uganda, AS Vita)
No comments:
Post a Comment