Valencia wakishangilia ushindi wao |
Ronaldo akifunga penati |
Ronaldo akikukuruka kuisaidia Real madrid ugenini kwa Valencia |
Real Madrid iliyokuwa imeshindwa mechi 22 mfululizo katika msimu huu ilizimwa na Milan na leo ikiwa ugenini licha ya kutangulia kupata bao katika dakika ya 14 kwa mkwaju wa penati lililofungwa na kinara wa mabao wa ligi hiyo, Cristiano Ronaldo ilishindwa kuhimili vishindo vya wenyeji wao.
Bao hilo lilikuwa la 25 kwa Ronaldo, baada ya Alvaro Negredo wa Valencia kuunawa mpira akiwa langoni mwake.
Wenyeji walirudi kipindi cha pili wakiwa wamecharuka na kujipatia bao la kusawazisha dakika ya 52 kupitia Barragan akimalizia kazi nzuri ya Jose Gaya kabla ya Nocolas Otamendi kuongeza bao la ushindi dakika ya 65.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo Atlético Madrid wakiwa nyumbani walipata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Levante, Sevilla ikiishinda Celta Vigo bao 1-0 nyumbani, Elche na Villarreal walitoka sare ya 2-2, huku Deportivo La Coruna wakiwa nyumbani waliitafuna Athletico Bilbao kwa bao 1-0 na Malaga kulala kwao mabao 2-1 dhidi ya Almería katika mechi zilizochezwa jana.
Kwenye nyingine za leo Getafe ikiwa nyumbani ililala mabao 2-1 dhidi ya Rayo Vallecano na kipigo cha Real Madrid kinaiweka katika nafasi ya kuenguliwa kileleni iwapo Barcelona inayotarajiwa kushuka dimbani hivi punde kama itaishinda Real Sociedad ya David Moyes watakaokuwa nyumbani kwao, kadhalika Espanyol itaikaribisha Eibar.
Real baada ya mechi 16 imesaliwa na pointi 39 Barcelona wenye michezo kama hiyo wakiwa na pointi 38 sawa na Atletico Madrid iliyotangulia kwa mchezo mmoja (17) wakiwa na pointi kama hizo 38.
No comments:
Post a Comment