Baadhi ya wanamuziki wa Sikinde, Hemba akiwa kati |
Akizungumza na MICHARAZO, mmoja wa viongozi wa Sikinde, Abdallah Hemba alisema kuwa, video hiyo itarekodiwa mara tu baada ya aalbamu yao kutolewa studio ilipokuwa inamaliziwa.
Hemba ambaye ni mmoja wa waimbaji waandamizi wa bendi hiyo, alisema ingawa mpaka sasa bado hawajaju kampuni itakayofanya kazi ya kuitengeneza video hiyo, lakini shughuli za kuirekodi itafanyika ndani ya mwezi huu wa Januari.
"Tutaanza kuirekodi mara baada ya albamu kutoka studio na tungependa kukamilisha mapema video hiyo kabla ya kumalizika kwa mwezi huu wa Januari ili kuachia kwa pamoja 'audio'," alisema.
Hemba alisema Sikinde imepania kutengenezea video nyimbo zote saba, japo ni chache zitakazoachiwa hewani ili kuitambulisha albamu hiyo yenye nyimbo kama 'Jinamizi la Talaka', 'Kibogoyo', 'Za Mkwezi', 'Nundu ya Ng'ombe', 'Kukatika kwa Dole Gumba', 'Deni Nitalipa' na 'Tabasamu Tamu'.
No comments:
Post a Comment