Yanga waliomaliza kibarua chao salama nchini Botswana |
Azam watakaoshuka dimbani leo nchini Sudan kujaribu kufuata nyayo za Yanga |
Na Rahma Junior
BAO la kufutia machozi lililofungwa na 'Uncle' Mrisho Ngassa, limeiwezesha Yanga kufuzu raundi ya kwanza ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Afrika, licha ya kipigo cha mabao 2-1 ilichopewa ugenini na BDF XI.
Goli la Ngassa aliyeiwezesha Yanga kuvuka hatua raundi ya awali na kwenda raundi kwa kwanza kwa jumla ya mabao 3-2,
baada ya kushinda 2-0 katika
mchezo wa kwanza uliochezwa jijini Dar es Salaam.
Ngassa alifunga bao hilo dakika ya 30 kuisawazishia Yanga waliompoteza Danny Mrwanda aliyepewa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa ya njano ya pili.
Wenyeji wlaitangulia kufunga bao kabla ya mchezaji wao mmoja kutolewa nje kwa kandi nyekundu kwa kumchezea rafu mbaya Simon Msuva.
Yanga sasa wanajiandaa kuvaana ama na Sofapaka ya Kenya au Plantinum ya Zimbabwe ambao wanarudiana leo mjini Harare baada ya wiki mbili zilizopita Wakenya kulala nyumbani mabao 2-1.Wawakilishi wengine wa Tanzania, Azam leo watakuwa kibaruani kuumana na Ekl Merreikh ya Sudan katika mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Azam imeifuata El Merreikh wakiwa na hazina ya ushindi wa mabao 2-0 iliyopata katika mechi wao wa kwanza uliochezwa uwanja wa Chamazi.
Azam inahitaji sare ya aina yoyote au hata kufungwa bao 1-0 kusonga mbele, na viongozi wa klabu hiyo wamenukuliwa wakitamba kuwa wapo kamili kwa vita.
Nazo timu za visiwani Zanzibar, KMKM leo itakuwa na kibarua kigumu cha kurudiana na Al Hilal ya Sudan waliowatandika mabao 2-0 wiki mbili zilizopita.
Wawakilishi wengine wa visiwani hiyo, Polisi wenyewe watashuka dimbani kesho kujaribu kurejesha mabao 5-0 iliyopewa na CF Mounama ya Gabon, jambo ambalo linaonekana kama ni ndoto.
No comments:
Post a Comment