STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, February 28, 2015

Simba kuvuna nini kwa Prisons, Ruvu wapo Mbeya

Simba watakaojiuliza kwa Prisons
Prisona watanusurika katika makucha ya Simba leo Taifa?

Ruvu Shooting watatoka salama uwanja wa Sokoine Mbeya?
Coastal Union kuendeleza ubabe kwa Mgambo JKT leo
KIVUMBI cha Ligi Kuu ya Tanzania Bara inaendelea tena leo kwa michezo mitano, 'Mnyama' Simba atakuwa dimba la Taifa, Dar es Salaam kujiuliza kwa Prisons Mbeya, wakati maafande wa Ruvu Shooting watakuwa uwanja wa Sokoine Mbeya kupepetana na Mbeya City.
Simba imetoka kukung;utwa baoa 1-0 na Stand United na ina pointi tatu tu toka kwenye mstari wa janga la kushuka daraja, kitu ambacho kimeanza kuwapa hofu mashabiki wao juu ya mwenendo wa timu yao.
Hata hivyo viongozi wamewatuliza mashabiki wao na kuwaambia Prisons hawatoki salama Taifa kwa kupata ushindi, huku maafande hao wakiwajibu kwa kuwaambia 'Thubutu!'
Prisons inaburuza mkia katika msimamo wa ligi hiyo na kocha wake David Mwamaja ameapa iwe isiwe leo ni lazima waue mnyama ili kukusanya pointi zitakazowatoa mkiani.
Maafande hao wana pointi 12 tu na wiki iliyopita iliikomalia Azam na kwenda nao sare ya bila kufungana ikiwa ni siku chache toka ikung'utwe mabao 3-0 na Yanga.
Mechi nyingine zinazochezwa leo ni pambano lililoanza kuzua gumzo kati ya Ruvu Shooting na Mbeya City litakalochezwa jijini Mbeya.
Tayarui Ruvu wameanza kuonyesha mchecheto kwa kudai wametishwa na 'vitendo' vya hujuma toka kwa wenyeji waom, japo wameapa kupambana ili kuvuna pointi kama walivyofanya Yanga wiki iliyopita.
Jijini Tanga kuna 'Tanga Derby' kati ya Mgambo JKT dhidi ya Coastal Union ambayo itashuka dimbani ikiwa chini hya kocha Jamhuri Kihwelu 'Julio' kwa mara ya kwanza.
Mchezo huo unachezwa kwenye uwanja wa Mkwakwani na Mgambo wanadeni la kipigo cha bao 1-0 walichopewa na wapinzani wao kwenye mchezo wa duru la kwanza.
Julio ametamba kuwa ameenda Coastal kurekebisha makosa na hasa kuwapa stamina wachezaji dosari aliyodai imeikwaza timu hiyo kutiosha, huku Bakar Shime wa Mgambo akisema awe Julio au James Nandwi wao wanataka kulipa kisasi na kujiweka pazuri baada ya kupoteza mechi mbili mfululizo.
Mjini Shinyanga nako kuna pambano la kutaka na shoka kati ya wenyeji Stand United dhidi ya 'wakuja' Kagera Sugar wanaoutumia uwanja wa Kambarage kama uwanja wao wa nyumbani baada ya kuukimbia CCM Kirummba Mwanza.
Tangu watue Shinyanga Kagera Suagr imekuwa ikipata ushindi wa  bao 1-0 na kuweza kukamata nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi hiyo nyuma ya vinara Yanga na Azam ambao wapo kwenye majukumu yao ya kimataifa katika michuano ya KOmbe la Shirikisho na Ligi ya mabingwa Afrika.
nazo timu za Polisi Moro na Mtibwa Sugar ambazo zimekuwa na matokeo ya siyoridhisha katika mechi zao zilizopita zitapepetana kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro katika pambano jingine la 'Derby'.
Mtibwa waliokuwa wakiongoza msimamo wa ligi kabla ya kurudi kichovu toka kwenye Kombe la Mapinduzi itakuwa na kazi kubwa kumalizana na Polisi Moro ambao mechi zao mbili zilizopita walipoteza baada ya kuwa na mwendo nzuri wa kugawa dozi kwa wapinzani wao.
Je ni timu ipi itakayocheza au kununa leo baada ya dakika 90 bila shaka ni jambo la kusbiri kuona.

No comments:

Post a Comment