STRIKA
USILIKOSE
Monday, May 18, 2015
Sunday, May 17, 2015
Wababe wa Yanga walala kwa waarabu wenzao
Kikosi cha Etoile du sahel |
Walipoumana na Yanga jijini Dar na kutoka sare ya 1-1 |
Etoile waliing'oa Yanga kwenye raundi ya pili kwa jumla ya mabao 2-1 ilikutana na kipigo hicho ugenini kupitia mabao ya kipindi cha kwanza.
Mabao hayo yaliwekwa kimiani na El Ouadi katika dakika ya 22 na Osaguona sekunde chache kabla ya mapumziko na kuwapa nafasi kubwa Wamorocco kunusa hatua ya makundi.
Hata hivyo Etoile bado wana nafasi ya kubadilisha matokeo watakaporudiana na wapinzani wao hao Juni 5 mjini Sousse, Tunisia.
Katika mechi nyingine za mtoano, Sfaxien ya Tuniais iliichapa ASEC Mimosas ya Ivory Coast kwa mabao 2-0, Stade Malien ikiwa nyumbani nchini Mali iliichjpa AS Vita ya DR Congo, Kaloum Star ya Guinea ilitandikwa nyumbani na Orlando Pirates ya Afrika Kusini Ijumaa kwa mabao 2-0.
Mechi nyingine ya mchujo huo zinachezwa jioni hii kwa timu ya Sanga Balende (DRC) kuvaana na Zamalek ya Misri, AC Leopard ya Kongo kuikaribisha Warri Stars ya Nigeria, watetezi Al Ahly ya Misri itavaana na Club Africans ya Tunisia na Esperance ya Tunisia kuialika Heart of Oak ya Ghana.
Hii ndiyo ratiba ya COSAFA 2015
Stars wanaoanza kazi yao kesho Cosafa |
Mei 17, 2015
Namibia v Shelisheli (Saa 9:00 Alasiri, Uwanja wa Moruleng)
Zimbabwe v Mauritius (Saa 11:30 jioni Uwanja wa Moruleng)
Mei 18, 2015
Lesotho v Madagascar (Saa 11:30 jioni Uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace)
Tanzania v Swaziland (Saa 1:30 usiku Uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace)
Mei 19, 2015
Shelisheli v Zimbabwe (Saa 11:00 jioni Uwanja wa Moruleng)
Namibia v Mauritius (Saa 1:30 usiku Uwanja wa Moruleng)
Mei 20, 2015
Madagascar v Tanzania (Saa 11:00 jioni Uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace)
Lesotho v Swaziland (Saa 1:30, usiku Uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace)
Mei 21, 2015
Namibia v Zimbabwe (Saa 11:00 jioni Uwanja wa Moruleng)
Shelisheli v Mauritius (Saa 11:00 jioni Uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace)
Mei 22, 2015
Lesotho v Tanzania (Saa 11:00 jioni Uwanja wa Moruleng)
Madagascar v Swaziland (Saa 11:00 jioni Uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace)
ROBO FAINALI
Mei 24, 2015
Ghana v Mshindi Kundi B (Saa 9:00 Alasiri Uwanja wa Moruleng)
Msumbiji v Malawi (Saa 11:30 Uwanja wa Moruleng)
Mei 25, 2015
Zambia v Mshindi Kundi A (Saa 11:30 Uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace)
Afrika Kusini v Botswana (Saa 1:30 usiku Uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace)
NUSU FAINALI ZA VIBONDE
Mei 27, 2015
Saa 11:00 jioni Uwanja wa Moruleng
Saa 1:30 usiku Uwanja wa Moruleng
FAINALI YA VIBONDE
Mei 29, 2015
Saa 11:00 jioni Uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace
NUSU FAINALI
Mei 28, 2015
Saa 11:00 jioni Uwanja wa Moruleng
Saa 1:30 usiku Uwanja wa Moruleng
MSHINDI WA TATU
Mei 30, 2015
Saa 9:00 Alasiri Uwanja wa Moruleng
FAINALI
Saa 11:30 jioni Uwanja wa Moruleng
Bale kuwaondoa RVP, di Maria Manchester Utd
Bale |
RVP na di Maria watampisha Bale Old Trafford? |
United inajiandaa kuwaacha Mholanzi, RVP na Muargentina, Di Maria aliyesajiliwa kwa kitita kikubwa msimu uliopita, ili kupunguza malipo ya mshahara wa Pauni 500,000 wanaopata nyota hao na kuwawezesha kumudu gharama za kumleta Bale kutoka Real Madrid.
Bale bado ameendelea kuwa katika mipango ya United katika usajili wa mwaka huu na inaaminika dili linaweza kukamilika na kumrejesha nyota huyo Ligi Kuu baada ya kukaa kwa kipindi cha miaka miwili Hispania.
Kabla ya kutimkia La Liga, Bale alikuwa akikipiga Tottenham Hotspur na kujijengea jina kubwa.
Uhakika wa United kumsajili Bale unatarajiwa kuifanya timu hiyo kuwaacha Van Persie na Di Maria ambao wote kwa pamoja na wanakunja kitita cha paundi 250,000 kwa wiki.
Yathibitika Andre Ayew Pele anukia England
RAIS wa klabu ya Marseille, Vincent Labrune amedai kuwa kuna uwezekano mkubwa wa Andre Ayew kutimkia katika Ligi Kuu ya England majira ya kiangazi.
Mkataba wa Ayew, nyota wa kimataifa wa Ghana katika klabu hiyo unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu na winga huyo ameweka wazi kuwa anataka kuondoka katika timu hiyo mwishoni mwa msimu huu.
Ayew mwenye umri wa miaka 25 aligoma kuweka saini ya mkataba mpya jambo ambalo lilizivuta klabu kadhaa kubwa barani Ulaya zikiwemo Manchester United, Arsenal na Liverpool.
Akihojiwa Labrune amesema pamoja na umuhimu wa Ayew katika kikosi chao, ila hawataweza kumbakisha kwasababu hawawezi kumpa ya fedha kama za klabu za Ligi Kuu ya England.
Labrune aliendelea kudai mfumo wa kifedha nchini Ufaransa ni tofauti, hivyo hawawezi kumpa fedha kama ambazo ataweza kuzipata akienda England.

Makocha 6 wawania kumrithi Goran Kopunovic Simba
Kocha Goran Kopunovic aliyepewa mkono wa Kwaheri Msimbazi |
Milovan anayetarajiwa kurudi Msimbazi |
Kocha Piet de Mol wa Ubelgiji anayetajwa kuja kuchukua mikoba ya Goran ndani ya Simba |
Hata hivyo uongozi huo tayari umeanza mchakato wa kusaka kocha mkuu mpya na tayari makocha sita toka nchi za Ujerumani, Ufaransa, Bulgaria, Serbia, Ubelgiji na Croatia wametuma maombi yao na uongozi wa Simba utaanza mchakato wa kupitia wasifu wa makocha hao kabla ya kumchukua mmoja.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zakaria Hanspope akiwa safari nje ya nchi aliiambia MICHARAZO kuwa, wameshindwana na Goran na sasa wanafanya taratibu za kumsaka kocha mpya ambaye atatangazwa mapema baada ya kupitiwa kwa wasifu wa makocha waliotuma maombi.
Hanspope alisema kuna orodha ya majina sita ya makocha toka barani Ulaya walioomba nafasi ya kumrithi Goran na utafanyika mchujo kabla ya kutoa jina moja la kubeba majukumu ya kuinoa Simba mpya kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
"Niko safarini, lakini taarifa nilizonazo ni kwamba tumeshindwana na Goran na tunasaka kocha mpya na tayari kuna majina sita yameshawasilisha maombi yao, kutoka nchi za Ubelgiji, Ufaransa, Serbia, Bulgaria na yatapitiwa wasifu wao na atakeyeenda na sifa ya klabu yetu tutamchukua," alisema Mwenyekiti huyo na kusisitiza kuwa ilikuwa ngumu kukubaliana na Goran juu ya masilahi.
"Goran alitaka masilahi makubwa ambayo klabu imeona isingeweza na tulimpa nafasi ya kujifikiria, lakini hata hivyo bado msimamo wake ulikuwa haujatulainisha kuafikiana naye, hivyo tumeachana naye na sasa tunaangalia mambo mengine," alisema.
Ingawa Hanspope alishindwa kutaja majina ya makocha hao walioomba kazi, lakini mmoja ya wanaotajwa kuwa na nafasi kubwa ya kumrithi Kopunovic ni Piet de Mol kutoka Ubelgiji ambaye ana rekodi na uzoefu wa soka la Afrika, huku Cirkovic Milovan akielezwa kuwa naye yu tayari kurudishwa katika kikosi hicho, huku akibebwa na rekodi zake kwa timu hiyo.
Juu ya usajili, zakaria Hanspope alisema ni mapema kwa sasa kwa sababu wanasubiri kwanza wapate kocha mpya ambaye atakuwa na mapendekezo yake, ingawa wameshaanza kuwasainisha wachezaji wao wa kikosi cha msimu ulioisha hivi karibuni.
STARS KUWAVAA SWAZILAND ROYAL BAFOKENG
Wachezaji wa Taifa Stars wakijifua mazoezini tayari kuanza kazi katika michuano ya COSAFA |
TIMU ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) itacheza mchezo wake wa kwanza wa
kombe la COSAFA siku ya jumatatu dhidi ya Swaziland katika uwanja wa
Royal Bafokeng pembeni kidogo ya jiji la Rustenburg kuanzia majira ya
saa 1:30 jioni kwa saa za Afrika Kusini.
Awali
michezo ya kundi B ilikuwa ifanyike katika uwanja wa Olympia Park,
lakini waandaji wa michuano ya COSAFA Castle wamesema kutokana na sababu
zilizopo nje ya uwezo wao michezo hiyo imeshindikana kufanyika katika
uwanja huo.
Uwanja
wa Royal Bafokeng ni miongoni mwa viwanja viliyotumika katika Fainali
za Kombe la Dunia 2010 chini Afrika kusini, ukiwa na uwezo wa kubeba
watazamaji 42,000 huku timu ya Platinum Stars iliyopo Ligi Kuu
ikiutumia kama uwanja wake wa nyumbani.
Leo
asubuhi Taifa Stars imefanya mazoezi katika uwanja wa shule ya
Rustenburg chini ya kocha mkuu Mart Nooij, na wachezaji wote wapo katika
hali nzuri kuelekea katika mchezo huo wa jumatatu.
Kesho
jioni Taifa Stars ifanya mazoezi saa jioni katika uwanja wa Rolay
Bafokeng kwa ajili ya kuuzoea uwanja kabla ya mchezo wenyewe dhidi ya
Swaziland.
Akiongelea
hali ya hewa, kocha mkuu wa Taifa Stars Mart Nooij amesema vijana wake
wanaendelea kuizoea hali ya hewa, japokuwa kuna baridi hakuna mchezaji
aliyeshindwa kufanya mazoezi kutokana na hali ya hewa.
Manchester Utd, Arsenal ni Ama Zao, Ama Zetu Englnad
LEO ndiyo Leo wakati wanaume 22 wa klabu za Manchester United na Arsenal watakapovaana katika pambano kali la Ligi Kuu ya England, huku kila timu ikihitaji ushindi ili angalau kujihakikisha nafasi ya pili ya msimamo wa ligi hiyo.
Pambano hilo litakalopigwa kwenye Uwanja wa Emirates limevuta hisia kali za mashabiki kutokana na ukweli timu zote zilipata matokeo tofauti katika mechi zao zilizopita. Arsenal inaifuata Mashetani Wekundu wakiuguza kichapo cha bao 1-0 walichopewa nyumbani na Swansea City wakati Mashetani hao wakichekelea ushindi wa ugenini dhidi ya Crystal Palace.
Arsenal waliopo nafasi ya tatu watahitaji ushindi huku wakiiombea mabaya waliokuwa mabibngwa watetezi manchjester Citrty watakaokuwa ugenini kuumana na Swansea kusudi warejeshe tumaini ya kukamata nafasi ya pili, nafasi kubwa kwa klabu hiyo kwa hivi karibuni kama wataipata mwisho wa msimu.
Mashetani wanaokamata nafasi ya nne nyuma ya Arsenal itakuwa ikihitaji ushindi ili kuipiku Wapiga Mitutu hao kwa tofauti ya pointi moja na kujiweka katika nafasi nzuri zaidi ya kurejea kwenye namba za juu ambazo msimu uliopita walizisikia redioni.
Mechi ya leo inakumbushia Robo Fainali ya Kombe la FA lililochezwa mwezi Machi na Arsenal kuwatoa nishai wapinzani wao kwa mabao 2-1.
Ukiachana na pambano hilo la leo, matokeo ya mechi zilizochezwa wikiendi hii ni kama ifuatavyo;
Liverpool ikiwa nyumbani ilikwanguliwa mabao 3-1 na Crystal Palace, huku
Southampton ikitafuna Aston Villa kwa mabao 6-1.
Matokeo ya mechi nyingine ni kama ilivyo hapo chini;
Burnley 0-0 Stoke
Queens Park Rangers 2-1 Newcastle United
Sunderland 0-0 Leicester City
Tottenham Spurs 2-0 Hull City
West Ham 1-2 Everton
Yanga kumburuza Kaswahili kwa kuwavuruga na Uchaguzi Mkuu
UONGOZI wa klabu ya soka ya Yanga umepanga kumburuza kwenye Kamati ya Maadili kwa mwanachama wao aliyejitambulisha kama Katibu wa Kamati ya Uchaguzi, Francis Kaswahili, juu ya Uchaguzi Mkuu wa klabu hiyo kinyume na taratibu. Uongozi wa Yanga umesema kuwa Kaswahili siyo Katibu wa kamati hiyo kwani kamati aliyokuwa akiiongoza ilishavunjwa, pia, hakutumwa na Sekratarieti ya Yanga na hat uanachama wake una walakini kwani siyo hai kwa miaka mingi. taarifa rasmi ni hiyo inayosomeka hapo juu. Kaswahili alitangaza Yanga ingefanya Uchaguzi wake mkuu Julai 12 mwaka huu japo ambalo uongozi umeruka kimanga. |
Friday, May 15, 2015
STARS YAENDELEA KUJIFUA BONDENI
Na Baraka Kizuguto, Afrika Kusini
Timu
ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imeendelea na mazoezi katika uwanja
wa Olympia Park kujiandaa na mchezo wa fungua dimba dhidi ya timu ya
Taifa ya Swaziland.
Kocha
mkuu wa timu ya Taifa Stars Mart Nooij amesema vijana wake wanaendelea
vizuri na mazoezi, ikiwa leo ni siku ya pili kufanya mazoezi baada ya
kufanya mazoezi ya kwanza jana jioni.
Nooii
amesema japokuwa kuna hali ya hewa ya baridi katika mji wa Rustenburg,
wachezaji wake wameanza kuizoea na kusema kwa kuwa bado kuna zaidi ya
masaa 72 kabla ya mchezo wa awali watakua wameshaizoea hali ya hewa.
Kuhusu
uwanja wa mazoezi, kocha Nooij amesema hali ya uwanja ni nzuri, uwanja
una nyasi nzuri hali inayopelekea kikosi chake kufanya mazoezi katika
mazingira mazuri.
Akiongelea
mchezo wake wa kwanza wa ufunguzi dhidi ya timu ya Taifa ya Swaziland
utakaochezwa siku ya jumatatu, amesema anawajua Swaziland ni timu nzuri,
mara ya mwisho katika mchezo wa kirafiki walitoka nao sare, hivyo
anawaanda vijana wake kupata ushindi katika mchezo huo.
Kikosi
cha Swaziland kina wachezaji mchanganyiko wakiwemo wanaocheza ligi yao
ya nyumbani na baadhi wanaocheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini.
Taifa
Stars itacheza mchezo wa kwanza dhidi ya Swaziland katika Uwanja wa
Olympia Park siku ya jumatatu saa 1.30 usiku kwa saa za huku, sawa na
saa 2.30 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Hapana! Ronaldo Kaongopa? Arukwa fedha za Nepal
SHIRIKA la Misaada la Save the Children limekanusha taarifa kuwa Cristiano Ronaldo ametoa msaada ya Euro Milioni 7 kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi nchini Nepal.
Kauli ya shirika hilo imekuja kufuatia taarifa kuwa Ronaldo mwenye umri wa miaka 30 ametoa kiasi hicho cha fedha kwenda kusaidia waathirika wa tetemeko hilo.
Katika taarifa ya shirika hilo imedai kuwa, Ronaldo akiwa Balozi wao amekuwa akipaza sauti kueleza matatizo wanayokutana nayo watoto duniani.
Lakini taarifa hiyo iliendelea kudai kuwa ripoti za hivi karibuni kuwa Ronaldo ametoa fedha kwa shirika hilo la Save the Children kwa ajili ya waathirika wa Nepal sio za kweli.
Zaidi wa watu 8,000 walifariki dunia kea tetemeko kubwa lililoikumba nchi hiyo Aprili 25 mwaka huu kabla ya lingine kutokea Mei 12 na kuua wengine karibu 110.

Monday, May 11, 2015
Mbeya City yawatunuku nyota wake, kocha Mwambusi
KLABU ya Mbeya City imewapa tuzo wachezaji wake pamoja na Kocha Juma Mwambusi kwa kuiwezesha timu hiyo kukamata nafasi ya nne katika Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2014-2015.
Tuzio hizo zilitolewa mara baada ya mchezo wao wa mwisho wa Ligi Kuu kati yao ya Polisi Moro ambapo Mbeya iliibuka washindi wa bao 1-0.
Kwenye tuzo hizo Kocha mkuu Juma Mwambusi alipata tuzo kama kocha mwenye mafanikio makubwa ndani ya kikosi cha city na ligi kwa ujumla Paul Nonga, Deus Kaseke, Themi Felix walipata tuzo ya heshima kwa kufanya vizuri misimu miwili Rafael Alfa na Kenny Ally walipata tuzo ya wachezaji chipukizi waliofanikiwa Haningtony Kalyusubula alipata tuzo ya mlinda lango bora na Juma Nyosso, Hassan Mwasapili na Peter Mwalyanzi walipata tuzo ya uchezaji bora
Halikadhalika wachezaji wengine 18 nao walipata zawadi ikumbukwe kuwa zawadi na tuzo hizo walizopata wachezaji wa City zimeambatana na bahasha iliyonona vizuri kutoka uongozi na mashabiki wa Mccfc.

Carlo Ancelotti ajipa matumaini kwa Juventus
MENEJA wa klabu ya Real Madrid, Carlo Ancelotti anaamini kikosi chake kinaweza kugeuza matokeo ya mabao 2-1 waliyochapwa na Juventus na kutinga hatua fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Pamoja na kutoka sare ya mabao 2-2 katika mchezo wa La Liga dhidi ya Valencia juzi. Mabingwa hao wa Ulaya sasa wako nyuma ya vinara Barcelona kwa alama nne huku kukiwa kumebaki michezo miwili katika ligi.
Akihojiwa kocha Ancelotti amesema wanahitaji kuwa mawazo chanya na kuthamini jinsi walivyocheza vyema katika mchezo huo.
Kocha huyo aliendelea kudai kuwa makosa madogo madogo ndio yaliyowagharimu, lakini wanahitaji kutulia na kujiandaa kwa ajili ya mchezo wao wa keshokutwa (Jumatano) dhidi ya Juventus.
Katika mfululizo wa michuano hiyo kesho Jumanne, Bayern Munich watakuwa nyumbani Alliaz Arena ikli kubadilisha matokeo ya mabao 3-0 iliyonyukwa katika mechi ya wiki iliyopita nchini Hispania.

Moyes anogewa La Liga, azipotezea klabu za EPL
AMENOGEWA! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya Meneja wa klabu ya Real Sociedad, David Moyes amezipasha klabu za Ligi Kuu zinazomuwinda kuwa hana mpango wa kwenda popote kufuatia tetesi kuwa atarejea nchini Uingereza.
Kocha huyo raia wa Scotland alitimuliwa na Manchester United baada ya kuinoa katika kipindi cha miezi 10, Novemba mwaka jana kutokana na klabu hiyo kutofurahishwa na matokeo.
Moyes alirejea tena uwanjani akiwa kocha wa klabu hiyo katika mazingira ambayo alikuwa hana mazoea nayo katika Ligi Kuu ya Hispania.
Wiki za karibuni kumezuka tetesi kuwa klabu za West Ham United na Newcastle United zimekuwa zikitaka saini yake, lakini mwenyewe amedai hana mpango wa kuondoka Hispania kwa sasa.
Akihojiwa Moyes amesema kwa sasa anataka kuimarisha kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao, jambo ambalo amefikia hatua nzuri hivyo hawezi kuacha mpaka azma yake itimie.

Maskini Dk Ndumbaro, TFF yakomaa naye!
Na Rahim Junior
TUMAINI la Mjumbe wa Bodi ya Ligi na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa klabu ya Simba, Dk Damas Ndumbaro kutoka kifungoni, limefifia baada ya Kamati ya Rufaa ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutupilia mbali rufaa yake.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Rufaa ya Nidhamu ya TFF, Revocatus Kuuli, inasema kwa maamuzi hayo yaliyofikiwa kwa turufu ya kura, ambapo wajumbe watatu waliafiki kupiga chini hoja za mrufani na mmoja kukubaliana naye ni kwamba, Ndumbaro ataendelea kutumikia adhabu yake kutojihusha na michezo kwa muda wa miaka saba.
Dk Ndumbaro alikata rufaa katika kamati hiyo kupinga maamuzi ya Kamati ya nidhamu iliyomkuta na hatia kwa kitendo chake cha kupinga maamuzi ya TFF ya kutaka klabu za Ligi Kuu kukatwa asimilia tano za fedha za wadhamini na kumtia kifungoni Oktoba mwaka jana.
Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa hizo za TFF ni kwamba baada ya mahojiano kati ya mrufani Dk Damas Ndumbaro na Wakili wa TFF, Emmanuel Muga, pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Rufaa ya Nidhamu iliamuriwa kutupiliwa mbali kwa hoja za mrufani kwa maamuzi ya kura 3-1.
"Kwa uamuzi huu kamati inadhibitisha uamuzi wa Kamati ya Nidhamu iliyosomwa Oktoba 13, 2014 uamuzi huu umefikiwa baada ya wajumbe kupiga kura na uamuzi kupitishwa kwa wingi wa kura za wajumbe watatu, dhidi ya mjumbe mmoja wa kamati hii kwa hoja ya 2,3 na 4 na wajumbe wote 4 walikubaliana kutupiliwa mbali hoja ya kwanza.
"Kwa hiyo Dk Damas Ndumbaro ataendelea kutumikia adhabu yake kwa kutojihusisha na shughuli yoyote ya Mpira wa Miguu (Soka) kwa kipindi cha miaka saba.
"Hata hivyo mrufani Dr Damas Ndumbaro anayohaki ndani ya siku 10 kuanzia leo Mei 10,2015 ya kuomba marejeo ya uamuzi huu mbele ya kamati ya Rufaa ya Nidhamu ya TFF chini ya Ibara 142 ya kanuni za nidhamu za TFF ya mwaka. " sehemu ya taraifa hiyo inasomeka hivyo.
Ebu isome taarifa hiyo ya Kamati ya Rufaa ya Nidhamu:
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAREHE 11 MEI 2015
MAAMUZI YA KAMATI YA RUFAA YA NIDHAMU
BAADA ya mahojiano kati ya mrufani Dr Damas Ndumbaro na Wakili wa TFF Nd Emmanuel Muga, pamoja na Wajumbe wa Kamati ya rufaa ya nidhamu kuwahoji wote, Mrufani na Wakili wa TFF, Kamati ya rufaa ya nidhamu ilichukua uamuzi ufuatao:-
Hoja ya kwanza cha rufaa, kwamba kamati ya nidhamu haikuwa na nguvu za kisheria kusikiliza shauri lake, Kamati ya rufaa ya nidhamu baada kusikiliza hoja za pande zote mbili, kwa uamuzi wa Wajumbe wote kwa maana ya kuwa zote nne za Wajjumbe wa kamati ya rufaa ya nidhamu, ilitupilia mbali hoja hiyo na kuona kwamba kamati ilikuwa na mamlaka ya kusikiliza shauri hilo kwa kuwa mkata rufaa ni afisa wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF kwa mujibu wa Katiba ya TFF ya 2013. Uamuzi katika hoja hii uliamuliwa kwa kura 3 dhidi ya moja.
Hoja ya pili inayosema kwamba kamati ilikosea kisheria kwa kutompa muda wa kuleta utetezi wake wala vielelezo vyovyote vile kwenye shauri lake.
Kamati ya rufaa ya Nidhamu kwenye Shauri hili, baada ya kufanya maamuzi kwa kupiga kura, kura za Wajumbe watatu zilitupiliwa mbali hoja yake na kura moja kati ya kura nne ilikubaliana na hoja yake kwa uamuzi huo, kamati ya rufani ya nidhamu ilitupilia mbali hoja hiyo kwa uamuzi wa wingi wa kura kwa maana ya kuwa tatu dhidi ya kura moja.
Sababu za kutupilia mbali hoja hizo ni kwamba mrufani alipata wito wa kwenda kwenye shauri, na akawakilishwa na wakili wake ( Nestory Peter Wandiba ) kwenye Shauri hilo. Shauri liliposikilizwa kwa mara ya kwanza tarehe 10/10.2014 shauri lilipangwa kusikilizwa tarehe 11/10/2014 Lakini siku hiyo ya pili si wakili wala Dr Ndumbaro alifika kwenye shauri hilo kwa maana hiyo basi shauri lililazimika kusilikizwa upande mmoja kwa mujibu wa kanuni za nidhamu za TFF ibara ya 94 (3).
3. Hoja ya tatu linalosema kwamba kamati ilikosea kusiliza shauri upande mmoja bila ya mtuhumiwa kuwepo, ni kukiuka haki yake ya msingi ya kusikilizwa.
Kamati baada ya kusikiliza utetezi kutoka pande zote mbili kamati ilifanya uamuzi kwa kupiga kura, na kura tatu (wajumbe watatu) walitupilia mbali hoja hiyo, dhidi ya kura moja (mjumbe mmoja) aliyeikubali hoja hiyo. Sababu za kutupilia mbali hoja hiyo ni kutokana na ukweli kwamba mrufani alipata wito wa kuhudhuria shauri hili na akamtuma wakili wake, lakini mrufani alishindwa kuonyesha vielelezo vya kuonyesha kwamba angesafiri kwenda nje ya nchi ili kamati ya nidhamu iweze kuahirisha shauri mpaka wakati ambao angekuwa amerejea lakini hakufanya hivyo.
Hata hivyo kwa mujibu wa Ibara 144(2) (3) za kanuni ya nidhamu za TFF, mrufani angeweza pia kuomba kamati ya nidhamu ibatilishe uamuzi iliyoutoa dhidi yake ili aweze kusikilizwa utetezi wake pia hakufanya hivyo na aliamua kukata rufaa.
4. Hoja ya nne inayosema kwamba kamati ilikosea kisheria katika uchambuzi wa ushahidi wa mlalamikaji na hatimaye kutoa uamuzi uliomtia hatiani.
Kamati ya rufani ya nidhamu ilisikiliza kwa umakini hoja za pande zote mbili na kujiridhisha kwamba mrufani alifanya makosa kwa kutoa taarifa isiyosahihi na kupotosha maamuzi ya TFF kinyume na kanuni ya 41 (6) ya kanuni za ligi kuu ya Tanzania toleo la 2014 (4) na pia kushawishi, kupotosha au kuzuia maamuzi/utekelezaji wa maamuzi ya TFF kinyume na kanuni ya 41(16) ya kanuni za ligi kuu za Tanzania ya (2014).
Wakati wa kufanya maamuzi, wajumbe watatu(3) kwa maana ya kura tatu zilitupilia mbali hoja hiyo, na kura moja, kwa maana ya mjumbe mmoja alikubaliana na hoja hiyo. Kwa maana hiyo, kamati ya rufaa ya nidhamu ya TFF imetupilia mbali hoja hiyo.
Kwa uamuzi huu kamati inadhibitisha uamuzi wa kamati ya nidhamu iliyosomwa tarehe 13/10/2014, uamuzi huu umefikiwa baada ya wajumbe kupiga kura na uamuzi kupitishwa kwa wingi wa kura za wajumbe watatu, dhidi ya mjumbe mmoja wa kamati hii kwa hoja ya 2,3 na 4 na wajumbe wote 4 walikubaliana kutupiliwa mbali hoja ya kwanza.
Kwa hiyo Dr Damas Ndumbaro ataendelea kutumikia adhabu yake kwa kutojihusisha na shughuli yoyote ya Mpira wa Miguu (Soka) kwa kipindi cha miaka saba.
Hata hivyo mrufani Dr Damas Ndumbaro anayohaki ndani ya siku 10 kuanzia leo tarehe 10/05/2015 ya kuomba marejeo ya uamuzi huu mbele ya kamati ya Rufaa ya Nidhamu ya TFF chini ya Ibara 142 ya kanuni za nidhamu za TFF ya mwaka.
Kila upande utabeba gharama zake Hukumu inasomwa leo tarehe 10/05/2015/
Revocatus L. K. Kuuli.
MAKAMU MWENYEKITI.
IMETOLEWA NA TFF

Sunday, May 10, 2015
Rasmi Kagame Cup kupigwa Dar kuanzia Julai 11-Agosti 02
HATIMAYE imefahamika kuwa, michuano ya Kombe la Kagame kusaka Bingwa wa Afrika Mashariki na Kati kwa ngazi za klabu itapigwa Tanzania.
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limekubali kuwa wenyeji wa michuano ya Kombe la Kagame baada ya kutafakari kwa kina.
Baraza la Vyama vya Soka kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) waliiteua Tanzania kuandaa michuano hiyo, lakini uongozi wa TFF, ulisema ungekutana kujadili kabla ya kutoa tamko.
Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa ya shirikisho hilo ilitolewa jana kwa vyombo vya habari TFF imethibitisha kuwa wamekubali kuandaa michuano hiyo na kutangaza kwamba itaanza kutimua vumbi lake kuanzia Julai 11 na kufikia tamati Agosti 2, mwaka huu.
TFF imeweka bayana kwamba Cecafa ndiyo itakayotangaza timu shiriki pamoja na ratiba nzima ya michuano hiyo ambayo mara ya mwisho kufanyika Tanzania ilikuwa mwaka 2012 ambapo Yanga ilitwaa taji kwa mara ya pili mfululizo kwa kuilaza Azam katika fainali iliyopigwa Uwanja wa Taifa. Mwaka mmoja nyuma yaani 2011 Yanga ilitwaa tena taji michuano ilipochezwa jijini Dar es Salaam kwa kuilaza Simba bao 1-0.
Bingwa mtetezi wa michuano hiyo kwa sasa ni wababe wa Azam, El Merreikh ya Sudan ambao walitwaa taji katika fainali zilizochezwa mwaka jana mjiji Kigali, Rwanda baada ya kuilaza APR bao 1-0.
Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika haya hapa
Watetezi wamewekwa kundi B |
Kundi B: Entente Setif (Algeria, mabingwa watetezi), USM Alger (Algeria), Al Merreikh (Sudan), MC Eulma (Algeria)
Mwanariadha Afa kwa Sumu India, wengine taaban
NEW DELHI, India
POLISI wa nchini India wanachunguza kifo cha
mwanariadha wa kike mwenye umri wa miaka 15 na wengine watatu wakinusurika kifo
baada ya kula kile kinachodaiwa matunda yaliyowekwa sumu, alisema waziri.
Ilielezwa kuwa wanariadha 10 walikula `othalanga’ matunda pori, ambayo
yaliwekwa katika vifungashio vyenye sumu katika kituo hicho cha michezo huko Alappuzha
kusini ya jimbo la Kerala kinachoendeshwa na Mamlaka ya Michezo India (SAI).
Wanariadha hao walikutwa wakiwa wamepoteza
fahamu katika hosteli yaol Jumatano jioni na walikimbishwa hospitalini ambako
mmoja wao alifariki dunia huku wengine watatu wakiwa katika hali mbaya.
Wote wanne inaaminika kuwa walisaini taarifa
ya kifo, walisema viongozi hao, lakini hakuna taarifa zaidi zilizotolewa kuhusu
barua hiyo.
Walisema ni mapema mno kuhisi kuhusu kifo cha
wanariadha hao chipukizi waliokuwa wakifanya mazoezi lakini ndugu wa waathirika
hao walisema kuwa wasichana hao walikuwa wameathirika kiakili kutokana na
kusumbuliwa na wanariadha wakubwa na makocha katika kituo hicho.
Waziri wa Vijana na Michezo Sarbananda
Sonowal alisema polisi wanachunguza na Mkurugenzi Mkuu wa SAI alikuwa akiongoza
taasisi hiyo pia.
"Sheria itachukua mkondo wake, lakini
nakuhakikishia kuwa kama kuna mtu yoyote kutoka katika mamlaka ya michezo
nchini India atapatikana na hatia kuhusiana na suala hili, atachukuliwa hatua
za kisheria mara moja," alisema Sonowal katika taarifa yake.
Mkurugenzi Mkuu wa SAI Injeti Srinivas aliwaambia
waandishi wa habari kuwa "ni tukio la kushtua sana ".
"Wasichana wanne walijaribu kujiua. Sasa
tunataka kuwapatia vifaa vya bora vya afya, " alisema.
Rais TFF awapo pole wahanga wa mafuriko
Rais wa TFF, Jamal Malinzi |
Na Rahma White
RAIS
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametuma
salamu za pole kwa wakazi wa Dar es salaam na hasa wale walioathirika na
mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es salaam kwa siku ya tatu
mfululizo sasa.
Katika
salamu zake kupitia kwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Mecky Sadik, Malinzi
amesema familia zimepoteza makazi, miundombinu ya usafiri na michezo
imeharibika na hata kuwa katika hali ya kutotumika, wanawake watoto,
familia, shughuli za kiuchumi na kimichezo zimeathirika na mvua hizi.
TFF inaunga mkono juhudi za Mkuu wa Mkoa Dar es salaam, Serikali na wadau wote wanaoshugulika kupunguza makali ya janga hili.
Polisi Moro, Masau Bwire warudi Ligi Daraja la Kwanza
Mbeya City wamemaliza kwa ushindi nyumbani dhidi ya Polisi |
Polisi wameenda na maji |
Yanga walioendelea kutoa takrima kwa timu pinzani |
Azam walimaliza kwa kishindo nyumbani |
JKT Ruvu licha ya kichaapo cha Simba wamenusuurika kushuka draja |
Ndanda wamepona baada ya kuilaza Yanga |
Simba waliomaliza ligi kwa kishindo kwa kuiparua JKT Ruvu |
Prisons wameponea chupuchupu |
Mtibwa wamemaliza kwa kichapo nyumbani mbele ya Coastal Union |
Ruvu inayonolewa na kocha Mkenya Tom Olaba ilikuwa ugenini Uwanja wa Kambarage
mkoani Shinyanga na kujikuta ikipokea kipigo cha bao 1-0 na wenyeji wao Stand
United ambayo ushindi huo umeifanya kufikisha pointi 31 katika nafasi ya 10.
Polisi Moro iliyopanda kucheza Ligi Kuu msimu huu, ilikubali kipigo cha
bao 1-0 kutoka kwa Mbeya City na kujikuta ikirudi ilipotoka na hiyo inatokana
na mwenendo wa kusuasua tangu kuanza kwa msimu huu ikiwemo uongozi kubadilisha
makocha mara kwa mara.
Polisi Moro ndiyo timu pekee msimu huu ambayo imefundishwa na makocha
watatu, ilianza na Adolf Rishard 'Adolf' kisha ikamfukuza na kumchukua Amri Said,
ambaye naye aliamua kujiondoa na nafasi yake kuchukuliwa na John Tamba, lakini
hadi siku jana walijikuta wakiburuza mkia wakiwa na pointi zao 25 katika mechi
26 walizocheza.
Katika uwanja wa Nang'wanda Sijaona mkoani Mtwara, Mabingwa wapya wa
msimu huu Yanga waliendelea kuonja shubiri baada ya kupoteza mchezo huo kwa
kufungwa bao 1-0 na wenyeji Ndanda FC, Wakati kwenye Uwanja wa Azam Complex
wenyeji Azam walitoka sare ya bila kufungana na Mgambo JKT ya Tanga.
Kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kocha, Mbwana Makatta,
alifanikiwa kuiokoa timu ya Tanzania Prisons isishuke daraja msimu huu baada ya
kuilazimisha sare ya bila kufungana na Kagera Sugar aliyomaliza nafasi ya sita
ikiwa na pointi 32, huku sare hiyo ikiwasaidia maafande hao kufikisha pointi 29
na kuepuka janga la kurudi kushuka daraja la kwanza msimu ujao.
Katika uwanja wa Manungu Turiani, Mtibwa Sugar ililala nyumbani kwa
kufungwa mabao 2-1 na Coastal Union ya Tanga na matokeo hayo kuifanya timu hiyo
iliyokuwa na kipindi kigumu licha ya kunza msimu huu vizuri kumaliza nafasi ya
saba msimu huu ikiwa na pointi 31 huku Wagosi wa Kaya wakimaliza nafasi ya tano
wakiwa na pointi 34.
Msimamo wa mwisho wa Ligi Kuu ya Bara:
P W D L F A Pts
1. Yanga 26 17 4 5 52 18 55
2. Azam 26 13 10 3 36 18 49
3. Simba 26 13 8 5 38 19 47
4. Mbeya City26 8 10 8 22 22 34
5. Coastal 26 8 10 8 21 25 34
6.Kagera 26 8 8 10 22 26 32
7. Mtibwa 26 7 10 9 25 25 31
8. JKT Ruvu 26 8 7 11 20 25 31
9. Ndanda 26 8 7 11 21 29 31
10.Stand 26 8 7 11 23 34 31
11. Prisons 26 5 14 7 18 22 29
12. Mgambo 26 8 5 13 18 28 29
13. Ruvu 26 7 8 11 16 29 29
14. Polisi Moro26 5 10 11 16 27 25
Matokeo:
JKT Ruvu v Simba (1-2)
Mtibwa Sugar v Coastal Union (1-2)
Stand Utd v Ruvu Shooting(1-0)
Mbeya City v Polisi Moro (1-0)
Kagera Sugar v Prisons (0-0)
Ndanda v Yanga (1-0)
Azam v Mgambo JKT (0-0)
WAFUNGAJI:
17- Simon Msuva (Yanga)
14- Amissi Tambwe (Yanga)
11- Abaslim Chiidiebele (Stand Utd)
10-Didier Kavumbagu (Azam)
Rashid Mandawa (Kagera Sugar)
Emmanuel Okwi (Simba)
9- Malimi Busungu (Mgambo)
8- Samuel Kamuntu (JKT Ruvu)
Ibrahim Ajibu (Simba)
Ame Ali (Mtibwa)
7-Rama Salim (Coastal)
6- Kipre Tchetche (Azam)
Danny Mrwanda (Yanga)
Heri Mohammed (Stand)
5- Jacob Massawe (Ndanda)
Yahya Tumbo (Ruvu)
Atupele Green (Kagera)
Mussa Mgosi (Mtibwa)
Nassor Kapama (Ndanda)
4- Ally Shomari (Mtibwa)
Themi Felix (Mbeya City)
Said Bahanuzi (Polisi Moro)
Frank Domayo (Azam)
Mrisho Ngassa (Yanga)
Kpah Sherman (Yanga)
Gaudence Mwaikimba (Azam)
Andrey Coutinho (Yanga)
Ramadhani Singano (Simba)
3- Dan Sserunkuma (Simba)
Elias Maguli (Simba)
Ally Nassor (Mgambo)
Raphael Alpha (Mbeya City)
Aggrey Morris (Azam)
Paul Nonga (Mbeya City)
NB:WAKILISHI WA NCHI, ZILIZOSHUKA DARAJA

Subscribe to:
Posts (Atom)