YAMETIMIA. Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) hatimaye limeufungia rasmi wimbo mpya wa nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Nay wa Mitego uitwao 'Shika Adabu Yako'.
Basata ilitangaza
hatua hiyo leo Ijumaa kupitia taarifa yake iliyosainiwa na Katibu Mtendaji
wake, Godfrey Mngareza, ikiwa saa chache tangu kuzagaa kwa taarifa hizo baada ya wimbo huo kuwa gumzo kupitia mitandao ya kijamii.
Katika wimbo huo
ulioachiwa mapema wiki hii, rapa huyo aliichana Basata katika moja ya mistari
yake na taarifa hiyo ya Basata imesema imeufungia wimbo huo kwa mujibu wa
mamlaka iliyonayo. Ikitumia kifungu cha 4 (1) (i) ya sheria namba 23 ya mwaka 1984 na kifungu cha 4 (2)
baraza hilo limetangaza kuupiga marufuku wimbo huo na kumpa onyo kali msanii
huyo.
"Tunafahamu
kuna wsanii wamekuwa wakifanya hivyo makusudi kutafuta umaarufu uchwara ambao
wanadhani utakuja kutokana na kuzungumzwa sana. Tunapenda kusema wazi kuwa
umaarufu hauji kwa upuuzi wa namna hiyo..."
Sehemu ya taarifa
hiyo ya Basata ilisomeka hivyo, ikifafanua pia imechukua hatua hiyo dhidi ya
wimbo huo kutokana na ukiukwaji mkubwa wa maadili, kashfa, uchochezi,
kudhalilisha watu na kuhatarisha amani na utengani miongoni wa wasanii na
jamii.
na kuzima tetesi
zilizotapakaa tangu juzi kuwa wimbo huo uliorekodiwa na Mr T Touch umefungiwa
kutokana na kuwa na mistari inayowananga wasanii mbalimbali akiwamo Wema, Ray,
Ommy Dimpoz, Shetta, DJ Choka na hata Basata lenyewe.
"Ujumbe huu
uwafikie Basata.....kazi kufungia nyimbo za wasanii, hivi mnajua tabu
tunazopata, mmeshindwa kazi kama mngekuwa watoto tungeshawachapa..."
Ni moja ya mstari uliopo kwenye wimbo huo ambao
umelalamikiwa na wasanii waliombwa na kuwagawa mashabiki wengine wakiuponda na
kuufagilia.
Basata imesisitiza pia kwa kumuonya msanii huyo kuwa makini katika kazi zake vinginevyo atachukuliwa hatua zaidi. Wa Mitego hakupatikana kusema lolote, lakini juzi alikakariwa kuwa hata kama wimbo utafungiwa basi wakubwa watakuwa wamechelewa kwa sababu kama ujumbe umeshafika kwa jamii na akitetea alichokiimba ni ukweli mtupu.
No comments:
Post a Comment