KAKATWA. Beki wa zamani wa Arsenal, Philippe Senderos ambaye amekuwa akihaha kurejea katika kiwango chake katika misimu ya karibuni, ameachwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Uswisi kwa ajili ya michuano ya Euro 2016.
Senderos ambaye ametumia muda mwingi msimu uliopita akiwa na timu yake ya nyumbani ya Grasshopper Zurich, alishindwa kuonyesha uwezo makeke ili kumshawishi kocha wake wakati Uswisi ilipotandikwa mabao 2-1 na Ubelgiji katika mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu.
Kocha Vladimir Petkovic ameamua kumuacha beki huyo mwenye umri wa miaka 31 licha ya hofu iliyopo kwenye ukuta wa timu hiyo baada ya Timm Klose na Johan Djourou kuwa nje kwa majeraha.
Beki wa Udenese Silvan Widmer na kiungo wa Basel Luca Zuffi aliyeonyesha uwezo mkubwa msimu huu pia wamekatwa katika kikosi hicho.
Uswisi inatarajiwa kucheza na Moldova katika mechi yake ya mwisho ya kujipima nguvu keshokutwa Ijumaa kabla ya kuvaana na Albania, Romania na wenyeji Ufaransa katika kundi A.
Kikosi Kamili
Makipa: Yann Sommer (Borussia Monchengladbach), Roman Burki (Borussia Dortmund), Marwin Hitz (Augsburg)
Mabeki: Stephan Lichtsteiner (Juventus), Nico Elvedi (Borussia Monchengladbach), Michael Lang (Basel), Johan Djourou (Hamburg), Steve von Bergen (Young Boys), Fabian Schar (Hoffenheim), Francois Moubandje (Toulouse), Ricardo Rodriguez (Wolfsburg)
Viungo: Valon Behrami (Watford), Blerim Dzemaili (Genoa), Gelson Fernandes (Rennes), Fabian Frei (Mainz), Granit Xhaka (Arsenal), Xherdan Shaqiri (Stoke City), Renato Steffen (Basel), Denis Zakaria (Young Boys)
Washambuliaji: Breel Embolo (Basel), Haris Seferovic (Eintracht Frankfurt), Admir Mehmedi (Bayer Leverkusen), Eren Derdiyok (Kasimpasa), Shani Tarashaj (Everton)
No comments:
Post a Comment