STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, June 9, 2016

Ronaldo, Messi hawashikiki kwa mkwanja mnene duniani

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgY8PvBrWzFoQIsf0lo44zBa1a5LOgQGVqaoJ90UrwDJJgXi6t_8HUQACiYEVoOsmc7yvAiWq9bU1MxejhpuojP57RhYySRr985IDkhFY-SDoKpnHzRkpsJcPrNdqi1JLmYe4aRX5wQzxo/s1600/lionel_messi_vs_cristiano_ronaldo.jpgWANANUKA pesa. Labda ubishe tu, lakini imefichuliwa kuwa nyota wanaochuana kwa sasa duniani, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo ndio wanamichezo wanaolipwa zaidi duniani.
Kwa mujibu wa Jarida maarufu la Forbes la Marekani limewataja nyota hao kuwa vinara duniani kwa kuvuta mkwanja wa maana wakiwazidi wanamichezo wengine.
Nyota wa Real Madrid, Ronaldo ndiye anayeongoza orodha hiyo kwa kukunja kitita cha Pauni Milioni 60.9 katika kipindi cha miezi 12 iliyopita, huku nyota wa Barcelona Messi akijikusanyia kiasi cha Pauni Milioni 56.3.
Mkali wa mchezo wa Gofu, Tiger Woods na bondia Floyd Mayweather ndio waliokuwa wakitawala orodha hizo kwa muongo mmoja uliopita, lakini Woods akiandamwa na majeruhi na kushuka kiwango na Mayweather akiwa amestaafu Ronaldo na Messi wamepanda na kuongoza orodha hiyo kilaini.
Ronaldo anakuwa mwanamichezo wa pili kutoka katika timu baada ya nguli wa mpira wa kikapu Michael Jordan kuongoza orodha hizo toka jarida hilo lilipoanza kukokotoa vipato vya nyota vya wanamichezo mbalimbali mwaka 1990.
Nyota wengine waliopo katika orodha hiyo ni nyota wa mpira wa kikapu Lebron James anayeshika nafasi ya tatu kwa kuingiza Pauni Milioni 53.4, nyota wa tenisi Roger Federer anashika nafasi ya nne akiingiza Pauni Milioni 46.9 na mkali mwingine wa Kikapu, Kevin Durant anakamilisha Tano Bora kwa kuingiza Pauni Milioni 38.6.
Mastraika matata kwa kufumania nyavu Neymar, Zlatan Ibrahimovic na Gareth Bale ndio wachezaji soka wengine pekee waliopo katika orodha hiyo wakiwa katika nafasi ya 21, 22 na 25 kwa kuingiza kiasi cha Pauni Milioni 25.8, 25.7 na 24.7.

No comments:

Post a Comment