Akianza matibabu |
zilipokuwa zikiondolewa kwa operesheni maalum |
Picha tofauti kuelekea kuziondoa tattoo zake usoni |
Alivyo sasa bila Tattoo |
Msela huyo kwa kutaka kujifanya anaenda na wakati alijichora tattoo kadhaa mwilini mwake, lakini mwishoni wa yote amejikuta akipata maumivu na kutoboka kiasi kikubwa cha fedha baada ya kufanyiwa upasuaji mara 25 ili kuzifuta tattoo hizo za usoni.
Inaelezwa jamaa huyo, Bryon Widner alitumia kiasi cha Pauni 20, 233 ambazo ni kama Shs. 63.9 Milioni, huku akisimulia namna alivyopata maumivu makali kwa ajili ya kusafisha uso wake kuondoa tattoo hizo.
Widner alisema kuwa, alipitia maumivu makali sana ili kusafisha sura yake na kuzitoa tattoo hizo na alitumia muda wa miezi 16 katika operesheni hizo 25 ili kuweka sawa sura yake.
Upasuaji huo wa kuondoa tattoo hizo za usoni kati ya tattoo kibao alizojichora mkora huyo ulifanywa na Dk Bruce Shack wa Vanderbilt University Medical Center kilichopo mjini Nashville.
Kitu cha kufutia ni kwamba licha ya kadhia zote hizo, kwa sasa Widner amesafishika sura yake akiwa hana kovu lolote usoni, jambo linalompa faraja.
No comments:
Post a Comment