MAELFU ya watu
wanatarajiwa kumuaga aliyekuwa bondia shupavu Muhammad Ali nyumbani
kwake katika mji wa Louisville huko Kentucky.
Bingwa huyo wa ndondi katika uzani mzito duniani na mwanaharakati alifariki siku ya Ijumaa akiwa na umri wa miaka 74.Umati mkubwa wa watu utachukua mwili wake na kuupitisha katika maeneo muhimu ya maisha yake kabla ya kuufanyia ibada.
Muingizaji Will Smith na aliyekuwa bondia Lenox Lewis watakuwa miongoni mwa wale watakaobeba jeneza lake ,huku aliyekuwa rais wa Marekani Bill Clinton akitarajiwa kutoa hotuba.
Muhammad Ali enzi za uhai wake siku za karibuni |
Miongoni mwa wale wanaotarajiwa kuhudhuria ibada ni rais wa Uturuki Reccep Tayyip Erdogan na mfamle Abdullah wa Jordan.
Rais Obama hatakuwepo,kwa kuwa anatarajiwa kuhudhuria sherehe ya kufuzu kwa mahafala ya mwanawe mkubwa Malia.Mshauri mkuu wa ikulu ya rais Valerie Jarret ambaye alimjua Ali atamwakilisha rais.
Lennox Lewis aliyekuwa bondia wa uzani mkubwa dunia kabla ya kustaafu kwake amesema kuwa ni heshimu kubwa kwake kuorodheshwa miongoni mwa wale watakaobeba jeneza la marehemu huku akisema kuwa kumbukumbu za Ali hazitasaulika.
Nyumbani kwa marehemu |
Ali alitaka ibada ya Janazah kuwa wakati wa mafunzo kulingana na Imam zaid Shakir alieongoza ibada hiyo.
Msomi wa Kiislamu Sherman Jackson alisema:Kufariki kwa Muhammad Ali kumetufanya tujisikie wapweke duniani.''Kitu kizima,kitu kikubwa na kinachovutia na kinachotoa uhakika wa maisha kimetuwacha''.
Baada ya kujiuzulu,uvumi ulianza kuhusu hali yake ya kiafya.Ugonjwa wa kutetetemeka mwili baadaye ulipatikana lakini Ali aliendelea kuwepo katika maeneo ya hadhara huku akipokewa vizuri kila anapoenda.
BBC
No comments:
Post a Comment