STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, June 10, 2016

Hizi ndizo rekodi za Mbeya City msimu wa 2015-2016

IMG_7987
Kikosi cha Mbeya City cha msimu uliopita
NA DISMAS TENI, MBEYA CITY
BAADA ya kumalizika kwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara  2015/16  na Mbeya City fc kumaliza ikiwa kwenye nafasi ya 8 baada ya kuweka kibindoni jumla ya Pointi 35,  kufuatia  mabao  32  ya kufunga na kufungwa 34 kwenye michezo 30 ya msimu mzima.
Hapa chini ni rekodi kadhaa kutoka benchi la ufundi zimetoka  na kati ya hizo baadhi  zinaonyesha kuwa, magolikipa watatu wa kikosi cha kwanza, Juma Kaseja, Haningtony Kalyesubula na Geoffrey Mwalyego  waliokuwa wakisimama langoni  kwa kupishana kwenye michezo tofauti wamewajibika kwa asilimia 33.33 katika ushindi, sare na hata kupoteza mchezo katika mechi zote 30 za msimu.
Katika rekodi hizo zinaonyesha,  Juma  Kaseja  alicheza michezo 17 na kuruhusu kufungwa mabao 20, Haningtony Kalyesubula alicheza michezo 13 na kufungwa mabao 14 wakati Geoffrey Mwalyego yeye hakupata nafasi ya kucheza mchezo hata mmoja.
Wakati Mlinzi Hassan Mwasapili akiweka rekodi ya kucheza mechi nyingi zaidi kikosini kuliko mchezaji yoyote kwa kucheza mechi 28 na kukosa 2  pia kufunga mabao 2  katika mechi zote 30, Mlinzi wa kati Haruna Shamte amemaliza akiwa na rekodi ya kupata kadi nyingi zaidi kuliko mchezaji yoyote akiwa na  jumla ya kadi 8, kati ya hizo 6 zikiwa za njano na 2 nyekundu.
Kiungo Rafael Daud ndiye kinara wa mabao kikosini akimaliza msimu kwa kufunga mabao 6,na kuifikia rekodi ya Mwegane Yeya aliyoiweka 2013/14,  ingawa  pia  ukurasa wake ukionyesha kuwa alipata kadi 2 za njano.
Mlinzi na kiungo Aboubakary Shaaban akiweka rekodi ya kucheza ligi kuu akiwa na umri mdogo zaidi kuliko wachezaji wote wa City, akicheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Coastal Union jijini Tanga akiwa na umri wa miaka 17 na siku 129.
David Kabole alicheza mechi 1 na kufunga bao 1 hii ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya JKT Ruvu ambao City ilipata ushindi wa 3-0 lakini baada ya hapo hakuonekana tena dimbani  hii ni baada ya kiwango chake kuporomoka kwa kasi na kujikuta akitolewa kwa mkopo kwenda Fc Kimondo na kumpisha Salvatory Nkulula  aliyeingia kikosini na kufanikiwa kucheza  mechi 6 akifunga mabao 4.
Rekodi pia  zinaonyesha 2015/16 ndiyo msimu  pekee ambao City imekuwa chini ya makocha watatu, ikianza na Juma Mwambusi  aliyeondoka  baadae, na nafasi yake kushikwa na Abdul Mingange  ambaye  alidumu kikosini kwa miezi 3, kufuatia matatizo ya kifamilia Mingane  aliachia nafasi hiyo na kumpisha kocha wa sasa Kinnah Phiri.
Licha ya kushinda 4-0 dhidi ya Coastal Union kwenye mchezo wa duru ya pili April 4 kwenye uwanja wa Sokoine jijini hapa, ushindi mkubwa wa City msimu huu ulikuwa ni ule wa bao 5-1 dhidi ya Toto Africans katika mechi ya kukata nashoka iliyopigwa jijini Mbeya, huku kipiko kikali kikiwa ni kile cha mabao 4-1 ilichokipa kutoka kwa Ndanda Fc huko Nangwanda Sijaona.
Katika nyota walisajiliwa wakati wa dirisha dogo Haruna Moshi  ameonekan kung’ara zaidi akifanikiwa kumaliza msimu akiwa amefunga mabao 3, sambamba na Ramadhani Chombo,Abdalah Juma na Ditram Nchimbi  waliofunga 2 kila mmoja ingawa Abdalah Juma hakumudu kuitumikia timu kwa kiwango kutokana na majereha ya mara kwa mara.
2015/16 ndiyo msimu pekee ambao City imeshinda mechi mbili pekee ugenini, 2-1 dhidi ya JKT Ruvu, Karume Dar na 1-0 dhidi ya Mgambo JKT, Mkwakwani, Tanga,  huku pia ikivuna pointi 3 za sare ugenini  dhidi ya Toto Africans, Coastal Union na Mwadui Fc.

No comments:

Post a Comment