STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, June 10, 2016

Kumekucha UEFA Euro Cup 2016! Nani kucheka?

https://i.ytimg.com/vi/cpdvLwDjjms/maxresdefault.jpg
PAZIA la michuano ya Fainali za Kombe la Ulaya 'UEFA Euro 2016' linafunguliwa rasmi leo kwa pambano moja tu la wenyeji Ufaransa dhidi ya Romania.
Pambano hilo linaashiria kuanza kwa vita ya kuwania taji la michuano hiyo ambalo kwa misimu miwili mfululizo limekuwa likishikiliwa na Hispania waliotwaa katika fainali za mwaka 2008 na 2012.
Ufaransa waliowahi kunyakua mara mbili taji hilo mwaka 1984 wakiwa wenyeji na 2000 nchini Ubelgiji/ Uholanzi ikiwa imetoka kutwaa Kombe la Dunia mwaka 1998 wakiwa pia wenyeji, inapewa nafasi kubwa ya kufanya kweli safari hii wakiwa kama wenyeji, lakini ni kutokana na kuwa na kikosi kinachoundwa na wachezaji mahiri na wajanja wa soka.
Hii ni mara ya tatu kwa nchi hiyo kuandaa fainali hizo baada ya ile ya kwanza mwaka 1960 na 1984, ambako kucheza kwenye viwanja vyake vya nyumbani na mashabiki watakaowatia nguvu na uimara wa kikosi chake ni dhahiri wakilikosa taji Ufaransa itabidi wajutue kwelikweli.
Pambano hili litakalopigwa majira ya saa 4;00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki, litatanguliwa na mashamsham ya uzinduzi kabla ya wanaume 22 kuonyeshana kazi kwenye dimba la Stade de France, Saint-Denis likihukumiwa na Mwamuzi Viktor Kassai kutoka Hungary.
pambano hilo la Kundi A linatarajiwa kuwa kivutio kikubwa kutokana na mafanikio makubwa ya vijana wa Ufaransa katika klabu zao kwenye Ligi Kuu tofauti za Ulaya akiwamo Paul Pogba ambaye kwa sasa amekuwa gumzo kutokana na kuwindwa na klabu kubwa duniani baada ya kutwaa mataji manne mfululizo ya Ligi ya Ufaransa.
Hata hivyo kama wenyeji wanapaswa kuwa makini dhidi ya Romania wanaoumana nao leo na hata washiriki wengine wa kundi hilo zikiwamo Uswisi na Albania.
Kipute cha michuano hiyo kitaendelea kesho Jumamosi kwa mechi tatu, moja ikiwa ya kundi A kati ya Uswisi na Albania itakayopigwa mapema saa 10 jioni na mbili za Kundi B.
Mechi hizo zitazikitanisha Wales dhidi ya Slovakia majira ya saa 1 jioni kabla ya England kuvaana na Russia saa 4 usiku, mechi zinazosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka duniani wakiwamo wa Tanzania.

Ratiba ilivyo kwa leo na kesho ikiwamo ile ya Kombe la Copa America ni hivi;
Leo Ijumaa
8:30 Usiku– Uruguay v Venezuela -Copa
11:00 Alfajiri– Mexico v Jamaica- Copa
4:00 Usiku– France vs. Romania-Uero

Kesho Jumamosi
8:00 Usiku– Chile v Bolivia-Copa
10:30 Alfajiri– Argentina v Panama-Copa
10:00 Jioni– Albania v Switzerland-Euro
1:00 Usiku– Wales    v. Slovakia-Euro
4:00 Usiku– England v Russia-Euro

No comments:

Post a Comment