Almas Kasongo aliyetetea kiti cha Uenyekiti wa DRFA |
SEHEMU kubwa ya uongozi uliokuwepo kwenye Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), akiwamo Mwenyekiti Almas Kasongo na Katibu Mkuu wake, Msanifu Kondo wamerejea madarakani baada ya kushinda kwenye uchaguzi uliofanyika leo.
Uchaguzi huo uliofanyika Hoteli ya Lamada, Ilala ilishuhudia Kasongo akitetea kiti chake mbele ya Peter Mhinzi na Emmanuel Kazimoto kwa kupata kura 12 dhidi ya 9 za Mhinzi ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Soka cha Temeke (TEFA).
Kondo akitetea kiti cha ukatibu Mkuu akimbwaga Frank Mchaki na Ramadhani Nassib, huku Mhazini aliyeongoza kiti hicho kwa muda mrefu, Ally Hassan akibwaga na Ally Masoud, huku Mtanganzaji na mchambuzi mahiri wa soka nchini, Shafii Dauda akitwaa Ujumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF.
Wengine waliochaguliwa ni Salum Mwaking'inda aliyeshinda nafasi ya Makamu Mwenyekiti, huku Michale Lupiana akishinda Uwakilishi wa Klabu na Amour Amour na Chichi Mwidege wakitwaa Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya chama hicho.
No comments:
Post a Comment