STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, December 2, 2014

Hivi ndivyo Diamond Platnumz alivyopokewa na tuzo zake 3














































PICHA ZOTE NA JESTINA GEORGE BLOG

Al Shaabab yawatimua Wakuu wa Usalama Kenya

Aliyekuwa Waziri wa Usalama, Joseph Ole Lenku
RAIS Uhuru Kenyatta amemwachisha kazi Waziri wa Usalama nchini Kenya, Joseph Ole Lenku na nafasi kumteua Joseph Nkaiseri, huku Mkuu wa Jeshi la Polisi,Inspekta Jenerali David Kimaiyo amejiuzulu wadhifa wake kutokana na shinikizo dhidi yake kutrokana na kudai kushindwa kutimiza wajibu wake kulinda Usalama nchini humo.
Rais Kenyatta alisema kuwa baada ya mazungumzo na Bw. Kimaiyo alikubali 'kustaafu' mapema kutoka kwa majukumu yake kwa sababu za kibinafsi.
Rais alitoa tangazo hilo wakati akihutubia taifa kufuatia shambulizi la hapo jana dhidi ya wachimba migodi 36 waliouawa na Al Shabaab mjini Mandera Kaskazini ya Kenya.
Rais pia alitangaza kuwa amekubali ombi la Generali wa polisi David Kimaiyo kuachia wadhifa wake. Kimaiyo na Ole Lenku wamekuwa wakikabiliwa na shinikizo za kuachia ngazi kufuatia kukithiri kwa utovu wa usalama nchini.
Hatua ya kuwatimua kutoka katika nyadhifa zao wawili hao bila shaka litakuwa jambo la kuridhisha kwa wakenya wengi ambao wamekuwa wakilalamikia utovu wa usalama na kuwataka waondoshwe ofisini. Uteuzi wa Joseph Nkaisery kama waziri mpya wa usalama ni jambo jipya kwani atakuwa mwanasiasa wa kwanza kutoka kwa upinzani kuwa ndani ya serikali.
Alipokuwa anahutubia nchi,Rais Kenyatta aliwasihi wabunge kuongeza muda wa vikao vyao vya leo ili kumhoji na kumkagua Nkaisery aliyeteuliwa kuchukua nafasi ya waziri mpya wa usalama na maswala ya ndani ili wamuidhinishe.

Make Money at : http://bit.ly/copy_win

Liverpool, Manchester Utd kuvuna nini leo EPL, Arsenal kesho

http://cdn.footballtarget.com/wp-content/uploads/2013/10/Manchester-United-vs-Stoke-City.jpghttp://assets.lfcimages.com/uploads/8847__0257__leicester_prem_away_1000x600_517X310.jpg 
VUMBI la Ligi Kuu ya England (EPL) linatarajiwa kutimika tena leo kwa michezo sita, ambapo klabu za Liverpool na Manchester United zitakuwa viwanja tofauti kusaka pointi tatu muhimu.
Liverpool ambayo imekuwa na mwenendo mbaya msimu huu itakuwa uwanja wa ugenini kuvaana na Leicester City, wakati Mashetani Wekundu walioanza 'kuchangamka' watakuwa Old Trafford kuialika Stoke City.
Mechi nyingine za leo itazikutanisha timu za Burnley itakayokuwa nyumbani kuikaribisha Newcastle United, Swansea City wataialika QPR, wakayi Crystal Palace itaikaribisha Aston Villa na West Bromwich Albion itaialika West Ham United katika mchezo mwingine mkali.
Mashabiki wa kandanda watakuwa na hamu ya kufuatilia pambano la Mashetani Wekundu ambao mwishoni mwa wiki wlaipata ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Hull City na kuingia kwenye Nne Bora.
Ingawa ushindi itakayopata leo timu hiyo inayonolewa na Mholanzi, Luis Van Gaal haiwezi kuwafanya wapande zaidi, lakini utawafanya wajichimbie zaidi katika nafasi hiyo ya nne kwani itafikisha pointi 25.
Moja pungufu ya ile ya Southampton ambayo wikiendi iliyopita ilitolewa nishai na Mabingwa watetezi Manchester City waliokwea hadi nafasi ya pili nyuma ya Chelsea.
Timu hizo zote tatu za Chelsea, Manchester City na Southampton zitashuka dimbani kesho kwenye mfululizo wa ligi hiyo maarufu duniani.
hiyo.
Liverpool baada ya kuzinduka mwishoni mwa wiki kwa kupata ushindi mwembamba dhidi ya Stoke City ni wazi wanahamu ya kuendeleza wimbi hilo ili kujenga imani kwa kocha Branden Rodgers.
Timu hiyo iliyomaliza katika nafasi ya pili msimu uliopita kwa sasa ipo nafasi ya 11 baada ya ushindi huo wa Jumamosi nyumbani, itahitaji kushinda leo licha ya kuwa uwanja wa ugenini na timu ambayo ilicharazwa maba0 3-2 na QPR na kuachwa mkiani.
Ligi hiyo itaendelea kesho kwa michezo minne, Arsenal itakuwa nyumbani uwanja wa Emirates kuikaribisha Southampton, Chelsea itaialika Spurs na City itaifuata Sunderland na Everton inayouguza kipigo cha mabao 2-1 ilichopewa ugenini na Spurs itaumana na Hull City.

Ajali Mlima Kitonga, basi latumbukia mtaroni na kuziba njia

 
Basi liitwalo Easy Bus lenye namba za usajili T 298 BLZ lililokuwa likitokea Lilongwe Malawi likiwa katika mtaro wa Mlima Kitonga.
 
 
Foleni kubwa iliyosababishwa na basi hilo baada ya kuingia mtaroni na kuziba njia.
BASI la abiria la Easy Bus lenye namba za usajili T 298 BLZ  linalofanya safari zake kati ya Malawi na Tanzania limepata ajali katika Mlima Kitonga, mapema leo baada ya kutumbukia kwenye mtaro.
Hata hivyo jambo la kushukuru Mungu ni kwamba hakuna mtu aliyepoteza maisha yake, japo ajali hiyo imesababisha foleni kubwa katika barabara hilo inayosifika kwa kona zake katika mlima huo.
Kwa mujibu wa mashuhuda, chanzo cha gari hilo kutumbukia mtaroni ni kufuatia kupata hitilafu na hatimaye uamuzi wa kuliegesha kando ukafanyika kisha abiria wote wakashuka ili kusubiri marekebisho hayo. 
Haikupita muda mrefu baada ya abiria kushuka gari lilikosa balansi, likaanza kurudi kinyumenyume na kisha kuingia mtaroni. 

Rais Kikwete amteua CAG mpya, ni Prof Mussa Juma Assad


cag_clip 
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Profesa Mussa Juma Assad kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Taarifa iliyotolewa, Jumatatu, Desemba Mosi, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, inasema kuwa uteuzi wa Bwana Assad ulianza Novemba 5, mwaka huu, 2014.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa Bwana Assad ataapishwa kesho, Jumanne, Desemba 2, saa nne asubuhi, Ikulu, Dar es Salaam.
Kabla ya uteuzi wake, Bwana Assad alikuwa Profesa Mshiriki, Idara ya Uhasibu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na anachukua nafasi ya Bwana Ludovick Utouh ambaye amestaafu kwa mujibu wa Sheria za Utumishi wa Umma.
Profesa Assad ni msomi, mwenye weledi, ujuzi na uzoefu mkubwa wa uhasibu na udhibiti wa fedha ambaye ana Shahada ya Uzamivu wa Uhasibu (PHD in Accounting) kutoka Chuo Kikuu cha Southampton, Uingereza mwaka 2001 na Shahada ya Uzamivu katika Udhibiti wa Fedha (MA in Financial Accounting) kutoka Chuo Kikuu cha Dublin City, Jamhuri ya Ireland mwaka 1991.Kusoma zaidi bofya
Profesa Assad pia ana Stashahada ya Kitaaluma ya Uhasibu (Professional Diploma in Accounting) kutoka Chuo Kikuu cha Dublin City mwaka 1990 na Shahada ya Biashara (Bachelor of Commerce) ya Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam mwaka 1988.
Pamoja na uzoefu wa kitaaluma, Profesa Assad anao uzoefu mkubwa katika eneo la uhasibu na ukaguzi. Alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA) kwa miaka saba (2007 – 2014); ni Rais na Mjumbe wa Chama cha Wahasibu Afrika (Pan African Federation of Accountants) tangu mwaka 2012; na ni mjumbe wa Bodi kadhaa za Wakurugenzi nchini Tanzania.
Katika kumteua Profesa Assad kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Rais anayo imani kubwa kuwa elimu, weledi, ujuzi na uzoefu ambao Profesa Assad anao utamwezesha kutekeleza vema majukumu ya nafasi hiyo muhimu sana katika utawala bora wa nchi yetu.

Irene Uwoya, JB, Richie kupamba uzinduzi Family Singers J'mosi

WASANII nyota wa filamu nchini, Irene Uwoya, Jacob Stephen 'JB' na Single Mtambalike 'Richie' wanatarajiwa kupamba uzinduzi wa albamu ya pili ya Kikundi cha Waimbaji wa Injili cha 'Family Singers' utakaofanyika siku ya Jumamosi.
Uzinduzi huo wa albamu hiyo iitwayo 'Usilie' utafanyika kwenye ukumbi wa PTA-Sabasaba, Temeke Dar es Salaam na utapambwa na shushuli za upimaji bure wa afya kwa wananchi mbalimbali sambamba na burudani ya muziki toka kwa waimbaji mbalimbali wa muziki wa Injili na wasanii hao wa Bongo Movie.
Mkurugenzi wa kikundi hicho kilichopo chini ya Kanisa la Waadventista wa Sabato (SDA), Daniel Misheto Jr, aliiambia MICHARAZO kuwa wasanii wa Bongo Movies wamethibitisha kuwapiga tafu katika uzinduzi huo ambao mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Misheto alisema kuwa maandalizi kuelekea uzinduzi huo yanaendelea vema na idadi wa watakaosindikiza ikizidi kuongezeka na kudai mbali na wasanii wa Bongo Movies, pia wazee wa Buguruni nao wamethibitisha kuwepo katika uzinduzi huo ambao utaenda sambamba na zoezi la kuwapima afya na kuwatibia watu bure kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 6 mchana kabla ya huduma ya uimbaji kushika kasi.
Baadhi ya waimbaji Injili watakaosindikiza onyesho hilo ni Leah Moody, mshindi wa BSS, Vocapella, Martha Mwaipaja, AIC (T) Vijana Chang'ombe, Accasia Singers, Papson Mistaki wa Kenya na Frank Hume kutoka Marekani.

Kun Aguero anyakua tuzo ya Mashabiki 2014

Sergio Aguero picked up Player of the Year award with girlfriend Karina Tejeda
Sergio Aguero akiwa na tuzo yake kwa pamoja na mpenzi wake, Karina Tejeda
STRIKA nyota wa klabu ya Manchester City, Sergio 'kun' Aguero ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Shirikisho la Mashabiki jana.
Mpachika mabao huyo wa mabingwa wa Ligi Kuu ya England na washindi wa pili wa Kombe la Dunia, Argentina, alishinda tuzo hiyo katika hoteli ya St Pancras Renaissance mjini London, England.
Nahodha wa Manchester United na England, Wayne Rooney na winga wa Real Madrid na Wales, Gareth Bale pia walikuwemo kwenye kinyang'anyiro cha tuzo hiyo sambamba na nyota wengine wa Ligi Kuu England, Thibaut Courtois, Branislav Ivanovic, Vincent Kompany, Pablo Zabaleta, Angel di Maria, Cesc Fabregas, Eden Hazard, Mesut Ozil, Yaya Toure, Sergio Aguero na Diego Costa.

BASATA yampongeza Diamond kwa kutwaa tuzo 3 za CHOMVA 2014

http://api.ning.com/files/Ct4BimYh7MjWwN3GDSYmz7wODwHWnN6B6NKofKrjboEN10YJnN3x6S3mquF1uzO9XyFNuVQVglyDwmavxGdZK*GQlLJBilOZ/04diamondtuzo4.jpgBARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) kama msimamizi na mratibu wa sekta ya Sanaa nchini linapenda kutoa pongezi za dhati kwa Msanii wa muziki wa kizazi kipya Nassib Abdul maarufu kama Diamond kwa kushinda tuzo tatu kwa mkupuo za CHOMVA zinazoendeshwa na kituo maarufu cha luninga cha Channel 0 chenye makao makuu yake Afrika Kusini.
Tuzo alizoshinda Diamond ni pamoja na Most Gifted East African Artist, Most Gifted Afro Pop video na ile ya Most Gifted New Comer. 
Kushinda kwa Diamond katika tuzo hizo kubwa barani Afrika na kuwashinda wasanii wengine wenye ‘majina makubwa’ ni ishara kwamba muziki wetu unakubalika ndani na 
Baraza linatoa wito kwa wasanii na wadau wote wa muziki kuzidisha ubunifu, bidii na weledi katika kazi wanazozifanya ili wasanii wengi zaidi waweze kuchomoza katika tuzo na majukwaa mbalimbali ya kimataifa kwa lengo la kujitangaza na kukuza soko la kazi zao kimataifa.
Aidha, Baraza linaendelea kuwakumbusha na kuwasisitiza wadau wa muziki na Sanaa kwa ujumla hususan wakuzaji Sanaa (mapromota) kuendelea kujenga mazingira rafiki kwa wasanii wetu kufanya kazi kwa ubora na weledi lakini pia kwa upendo na furaha ili kujenga daraja zuri kwa wasanii wengi zaidi kung’ara kwenye ngazi za kimataifa.
Ni imani ya Baraza kwamba, ushindi huu wa kihistoria wa Diamond utakuwa chachu kwa wadau wote wa Sanaa nchini hususan wasanii katika kujituma na kuhakikisha hawaridhiki na mafanikio waliyonayo. 
Ni matumaini ya Baraza kwamba wasanii na wadau wote wa Sanaa wataendelea kutambua umuhimu wa kufuata sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji sekta sambamba na kutambuliwa na Serikali.
Sanaa ni kazi, tuipende na kuithamini