STRIKA
USILIKOSE
Tuesday, December 2, 2014
Liverpool, Manchester Utd kuvuna nini leo EPL, Arsenal kesho
VUMBI la Ligi Kuu ya England (EPL) linatarajiwa kutimika tena leo kwa michezo sita, ambapo klabu za Liverpool na Manchester United zitakuwa viwanja tofauti kusaka pointi tatu muhimu.
Liverpool ambayo imekuwa na mwenendo mbaya msimu huu itakuwa uwanja wa ugenini kuvaana na Leicester City, wakati Mashetani Wekundu walioanza 'kuchangamka' watakuwa Old Trafford kuialika Stoke City.
Mechi nyingine za leo itazikutanisha timu za Burnley itakayokuwa nyumbani kuikaribisha Newcastle United, Swansea City wataialika QPR, wakayi Crystal Palace itaikaribisha Aston Villa na West Bromwich Albion itaialika West Ham United katika mchezo mwingine mkali.
Mashabiki wa kandanda watakuwa na hamu ya kufuatilia pambano la Mashetani Wekundu ambao mwishoni mwa wiki wlaipata ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Hull City na kuingia kwenye Nne Bora.
Ingawa ushindi itakayopata leo timu hiyo inayonolewa na Mholanzi, Luis Van Gaal haiwezi kuwafanya wapande zaidi, lakini utawafanya wajichimbie zaidi katika nafasi hiyo ya nne kwani itafikisha pointi 25.
Moja pungufu ya ile ya Southampton ambayo wikiendi iliyopita ilitolewa nishai na Mabingwa watetezi Manchester City waliokwea hadi nafasi ya pili nyuma ya Chelsea.
Timu hizo zote tatu za Chelsea, Manchester City na Southampton zitashuka dimbani kesho kwenye mfululizo wa ligi hiyo maarufu duniani.
hiyo.
Liverpool baada ya kuzinduka mwishoni mwa wiki kwa kupata ushindi mwembamba dhidi ya Stoke City ni wazi wanahamu ya kuendeleza wimbi hilo ili kujenga imani kwa kocha Branden Rodgers.
Timu hiyo iliyomaliza katika nafasi ya pili msimu uliopita kwa sasa ipo nafasi ya 11 baada ya ushindi huo wa Jumamosi nyumbani, itahitaji kushinda leo licha ya kuwa uwanja wa ugenini na timu ambayo ilicharazwa maba0 3-2 na QPR na kuachwa mkiani.
Ligi hiyo itaendelea kesho kwa michezo minne, Arsenal itakuwa nyumbani uwanja wa Emirates kuikaribisha Southampton, Chelsea itaialika Spurs na City itaifuata Sunderland na Everton inayouguza kipigo cha mabao 2-1 ilichopewa ugenini na Spurs itaumana na Hull City.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment