KIKOSI
cha pili cha timu ya taifa, maarufu kama Taifa
Stars Maboresho kimeingia kambini Bulyanhulu
mkoani Shinyanga kujiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Burundi
itakayochezwa Desemba 9 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Ikiwa
chini ya Kocha Mart Nooij, Stars Maboresho itapiga kambi mkoani humo
hadi Desemba 6 mwaka huu ambapo itarejea jijini Dar es Salaam tayari kwa
ajili ya mechi hiyo itakayochezwa Uwanja wa Taifa.
Wachezaji
walioingia kambini ni Abubakar Ally (Coastal Union), Abubakar Ally
Mohamed (White Bird), Aishi Manula (Azam), Andrew Vicent (Mtibwa Sugar),
Atupele Green (Kagera Sugar), Edward Charles (Yanga) na Emmanuel
Semwanda (African Lyon).
Gadiel
Michael (Azam), Hashim Magoma (Stand United), Hassan Banda (Simba),
Hassan Mwasapili (Mbeya City), Joram Mgeveke (Simba), Kassim Mohamed
Simbaulanga (African Lyon), Kelvin Friday (Azam) na Makarani Ally
(Mtibwa Sugar).
Miraji
Adam (Simba), Mohamed Hussein (Simba), Muzamir Ally (Mtibwa Sugar),
Omari Nyenje (Ndanda), Pato Ngonyani (Yanga), Rashid Mandawa (Kagera
Sugar), Said Hamisi (Simba), Salim Hassan Mbonde (Mtibwa Sugar) na Shiza
Ramadhan (Mtibwa Sugar).
Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF) linaishukuru kampuni ya kuchimba madini ya
Acacia Mining PLC (zamani African Barrick Gold PLC) kwa kufadhili kambi
ya Stars kupitia mgodi wa Bulyanhulu.
No comments:
Post a Comment