STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, December 2, 2014

Klabu za Simba, Yanga zapigwa vijembe

http://ehabari.com/wp-content/uploads/2014/12/7a19Simba-Yanga.jpgUONGOZI wa Ruvu Shooting umezipiga 'madogo' klabu za Simba na Yanga kwamba zimekuwa mahiri katika kuviza vipaji vya soka vya wachezaji nchini kutokana na kuwasajili kwa papara kila wanapong'ara katika timu nyingine, kisha kushindwa kuwatumia.
Aidha uongozi huo umewazindua wachezaji vijana kuwa makini na kuzikimbilia klabu hizo hata kama ni kweli zina masilahi makubwa miongoni mwa klabu za soka za Afrika Mashariki, lakini ni vema pia wakaangalia vipaji vyao.
Akizungumza na MICHARAZO, msemaji wa Ruvu Masau Bwire, alisema Simba na Yanga ni klabu za 'kuviza' vipaji ndiyo maana asilimia kubwa ya wachezaji waliokuwa nyota katika klabu zao wanaposajiliwa na klabu hizo hufifia na hata kuzimika kama baadhi yao ambao licha ya kusajiliwa kwa mamilioni ya fedha wamekuwa watu wa kukaa benchi.
"Ni lazima wachezaji wanaozikimbilia Simba na Yanga wajiulize mara mbili, ni kweli zina mvuto wa kifedha lakini vipaji vyao ni muhimu, kuna maana gani kusajiliwa kwa mamilioni ya fedha kisha ukaishia kukaa benchi na mwishowe kutemwa ukiwa haina thamani," alihoji.
Bwire alisema wapo wachezaji kadhaa waliokuwa waking'ara nje ya Simba na Yanga, lakini walipotua katika timu hizo wamekuwa hawana maana yoyote wakiishia kuwa wasugua benchi kisha kuachwa kwa kudaiwa kushuka viwango na wanaposajiliwa na timu nyingine zinazowapa nafasi ya kucheza hurejea kwenye viwango vyao na klabu hizo kubwa kuwavizia tena kutaka kuwasajili.
Baadhi ya wachezaji wamekuwa wakizikimbilia Simba na Yanga kwa sababu ya usajili wa donge nono, lakini mrundikano wa wachezaji wengi mastaa umewafanya kuishia kukalia benchi na kushuka viwango kabla ya kutemwa, kitu kinachodaiwa kinachangia kudidimiza soka la Tanzania.

No comments:

Post a Comment