STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, January 26, 2014

TPBO-Limited yaitisha mkutano wa wadau wa ngumi jijini Dar


WADAU wa ngumi za kulipwa nchini wanatarajia kukutana katika mkutano wa pamoja ulioitishwa na Oganaizesheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBO-Limited) ili kujadili mustakabali wa mchezo huo kwa mwaka 2014.
Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu wa Oganaizesheni hiyo, Ibrahim Kamwe mkutano huo utafanyika kwenye ukumbi wa Vijana Social, Kinondoni na utahudhuriwa na wadau wote wa ngumi hizo nchini.
Miongoni mwa wadau ambao ndiyo walengwa wakuu wa mkutano huo uliofadhiliwa na Kitwe Traders ni;  makocha, mabondia, mapromota, waamuzi na watu wote ambao wamekuwa bega kwa bega na mchezo huo.
Kamwe alisema  lengo kuu la mkutano huo ni kujadili namna ya kuupelekea mbele mchezo huo ambao pamoja na kutokuwa na wadhamini, lakini dniyo ambao umekuwa ukiiletea sifa Tanzania kwa mabondia wake kunyakua mataji ya kimataifa.
Alisema wamewaalika pia viongozi wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na wadau wengine wakiwamo viongozi wa mashirikisho ya ngumi hizo nchini kama akina Emmanuel Mlundwa wa PST, Onesmo Ngowi wa TPBC.
"Mkutano huo utahudhuriwa na wadau wengine wakiwemo makondia wastaafu kama akina Matumla, Habib Kinyogoli, Names Kavishe, Zuwena Kibena na wadau ambao wamekuwa wakiusaidi kusonga mbele ili tujadili na kupanga mikakati ya mwaka 2014," alisema Kamwe.
Alitoa wito kwa yeyote ambao anajitambua kuwa ni mdau wa ngumi za kulipwa nchini wakipata taarifa yake wasisite kujitokeza kwenye ukumbi wa mkutano huo kwa lengo la kufanikisha yale wanayotaka yawe.

Hivi ndivyo PSPF ilivyonogesha tuzo za mabondia jana

Meneja Mpango wa Uchangiaij wa hiyari kutoka PSPF ,Mwanjaa Sembe kushoto akimpatia ya upiga picha bora wa mchezo wa masumbwi pamoja na uhamasishaji mchezo huo Rajabu Mhamila 'Super D' wakati wa utoaji wa Tuzo hizo kwa mabondia zilizofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es  salaam picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Naibu Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Juma Mkamia akimkabidhi tuzo ya bondia bora wa mwaka 2013 kwa ngumi za ridhaa  Gelvars Rogasian wakati wa utoaji tuzo za PSPF BOXING AWARDS zilizofanyiaka katika ukumbi wa PTS Sabasaba picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Naibu Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Juma Mkamia akimkabidhi tuzo ya bondia bora wa mwaka 2013 kwa ngumi za kulipwa  Francsis Cheka wakati wa utoaji tuzo za PSPF BOXING AWARDS zilizofanyiaka katika ukumbi wa PTS Sabasaba picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Mjumbe wa maendereo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini Aisha Vonialis kulia akiwa na Naibu Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Juma Mkamia
picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Mjumbe wa maendereo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini Aisha Vonialis kulia akiwa na Fransic Cheka
picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Mjumbe wa maendereo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini Aisha Vonialis kulia ajkiwa na Zuwena Kipingu ambaye ni Mjumbe wa shilikisho la ngumi za ridhaaa nchini BFT picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Tuzo iliyochukuliwa na Rajabu Mhamila Super d
Rais wa PST Emanuel Mlundwa kushoto akimpatia tuzo ya Bondia bora wa mwaka Bilali Ngonyani kwa niaba ya Ibrahimu Class King Class Mawe

Aga Peter akimpatia tuzo Franscis Cheka

Mdau wa masumbwi Aga Peter akimkabidhi tuzo Fadhili Majia kulia ni Mjumbe wa maendereo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini Aisha Vonialis
picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Promota wa masumbwi Mohamed Bawazir akimpatia tuzo ya uandishi bora wa mchezo wa masumbwi Mwali Ibrahimu katikati ni Mjumbe wa maendereo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini Aisha Vonialis
picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Rashidi Matumla akimpatia tuzo Fadhili Majia


Mjumbe wa maendereo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini Aisha Vonialis kulia ajkiwa na Zuwena Kipingu ambaye ni Mjumbe wa shilikisho la ngumi za ridhaaa nchini BFT wakipiga picha ya pamoja na hadija Khopa picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

kocha wa timu ya Taifa Jonas Mwakipesile akimkabidhi tuzo Selemani Kidunda
picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Mjumbe wa maendereo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini Aisha Vonialis kushoto akimkabidhi tuzo kocha wa timu ya Taifa Jonas Mwakipesile picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Logarusic katika mtihani wa kwanza Ligi Kuu Bara

Logarusic kocha wa Simba

BAADA ya kutua kwa mbwembwe na kuiwezesha Simba kunyakua taji la Nani Mtani Jembe kisha kulikosa kiduchu Kombe la Mapinduzi, Kocha Logarusic Zdravko ataanza rasmi kibarua chake katika  Ligi Kuu Tanzania Bara leo wakati vijana wake watakapovaana na Rhino Rangers.
Kocha huyo kutoka Croatia, aliajiriwa Simba kwa mkataba wa miezi sita kuchukua nafasi ya Abdallah Kibadeni 'King' aliyeiwezesha timu hiyo kushika nafasi ya nne kwenye hatua ya duru la kwanza la ligi hiyo iliyokuwa imesimama na kuanza rasmi jana kwa mechi kadhaa.
Hivyo pambano la Simba na Rhino litakalochezwa kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni mtihani wa kwanza kwa kocha huyo ambaye mechi zake mbili zilizopita alishuhudia vijana wake wakigaragazwa.
Baada ya kushinda mfululizo, Simba ilisimamishwa na KCCA ya Uganda kwa kufungwa bao 1-0 kwenye pambano la fainali za Kombe la Mapinduzi lililochezwa mjini Zanzibar kabla ya wiki iliyopita kulazwa tena 1-0 na Mtibwa Sugar katika pambano la kirafiki lililochezwa jijini Dar.
Lugarusic aliingia Msimbazi kwa kismati kwa kuitandika KMKM ya Zanzibar kwa mabao 3-1 kabla ya kupata ushindi kama huo kwa Yanga na baadaye kwenda Zenji na kufanya vema kabla ya kufungwa na KCCA.
Simba itaikaribisha Rhino waliotoshana nao nguvu kwa kutoka sare ya 2-2 mjini Tabora katika mechi yao ya awali, ikiwa na nyota wapya watano, Donald Musoti wa Kenya, Ivo Mapunda, Ali Badru aliyekuwa Misri, Awadh Juma wa Mtibwa na kipa Yew Berko wa Ghana.
Pia itakuwa na kiungo wake wa zamani, Uhuru Suleiman aliyekuwa akiichezea Coastal Union kwa mkopo kwenye duru la kwanza ambaye ataungana na wakali wengine kuanza mbio za kuufukia ubingwa wa ligi hiyo unaoshirikiliwa na watani wao Yanga.
Mbali na mechi hiyo ambayo mashabiki wana hamu ya kutaka kuona Simba chini ya kocha Logarusic wataanza vipi, pia leo kuna pambano jingine ambalo litazikutanisha timu za maafande wa JKT Ruvu itakayoikaribisha Mgambo JKT ya Tanga kwenye uwanja wa Chamazi.
Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea tena siku ya Jumatano kwa mechi tano ambazo zitazikutanisha timu 10 ambapo moja ya mechi hizo ni Kagera Sugar itakuwa nyumbani kwao mjini Bukoba kuikaribisha 'ndugu' zao Mtibwa Sugar.
Michezo mingine ya siku hiyo ni ile ya Azam Fc dhidi ya Rhino Rangers, Ruvu Shooting kuialika Mbeya City kwenye uwanja wa Mabatini huku watetezi Yanga 'Wazee wa Uturuki' watawafuata Coastal Union iliyokea Oman katika jiji la Tanga.

Juan Mata rasmi Manchester United kuanza kukipiga Jumanne

75040_10151963634432746_2072552034_n
Manchester United imekamilisha rasmi usajili wa kiungo Juan Mata kutoka Chelsea kwa ada ya usajili ya £37.1 million, ambayo ni rekodi mpya katika usajili wa United, klabu hiyo imethibitisha.
Mata, 25, ameshaichezea mara 32 timu ya taifa ya Spain na amecheza mechi  Chelsea, akifunga mabao 32 tangu alipojiunga na klabu hiyo akitokea Valencia mwaka 2011.
Juan Mata alinukuliwa na mtandao wa Man U akisema: “Nina furaha sana kujiunga na United. Nilikuwa ni muda mzuri sana Chelsea lakini muda umefikia kwa changamoto mpya. United ni sehemu sahihi kwangu na nina shauku kubwa ya mmoja ya waliopo katika historia mpya ya klabu hii.
“Chelsea ni timu kubwa na nina marafiki wengi pale lakini huwezi kukataa nafasi ya kujiunga na Manchester United.” – Mata

HII NDIYO RATIBA KAMILI YA DURU LA PILI LIGI KUU TANZANIA BARA


Januari 25, 2014
Ashanti Utd   vs   Yanga SC
Azam FC    vs Mtibwa S
Coastal U    vs JKT Oljoro
Kagera S    vs Mbeya City
Prisons  vs R.Shooting 
 

Januari 26, 2014
JKTRuvu    vs Mgambo
Simba SC    vs Rhino
***********

Januari 29, 2014
Kagera S    vs Mtibwa  

 Azam FC    vs Rhino
Prisons    vs JKTRuvu
Ruvu Shooting   vs Mbeya City
Coastal U    vs Yanga SC 
Februari 1, 2014
Ashanti Utd   vs Mgambo
Simba SC    vs JKT Oljoro 
**********
Februari 2, 2014
Yanga SC  vs Mbeya City
Prisons    vs Coastal
Mgambo   vs  Ruvu Shooting
Azam FC    vs Kagera Sugar
Februari 5, 2014
Mtibwa S    vs Simba SC
Rhino     vs  JKT Oljoro
JKTRuvu    vs Ashanti Utd 
************
Februari 9, 2014
Mgambo     vs  Simba SC
JKT Oljoro   vs Kagera S
Rhino     vs  Coastal U
Mbeya City   vs Mtibwa
JKTRuvu    vs R.Shooting
Februari 15, 2014
Rhino     vs  Mgambo
Ashanti Utd   vs Kagera
***********
Februari 15, 2014
Mtibwa S    vs Prisons
JKT Oljoro   vs JKTRuvu
Mbeya City   vs Simba SC
Ruvu Shooting   vs Coastal U 
Februari 22, 2014

Ruvu Shooting   vs Yanga SC
Kagera S    vs Rhino
Mtibwa S    vs Ashanti Utd 
************
Februari 22, 2014
Coastal U  vs Mbeya City
JKT Oljoro   vs Mgambo
Azam FC    vs Prisons
Februari 23, 2014
Simba SC    vs JKTRuvu 
Februari 26, 2014
Yanga SC    vs Prisons
Ashanti Utd   vs Azam FC 
Machi 2, 2014
Simba SC    vs R.Shooting 
*************
Machi 2, 2014
Kagera S    vs JKTRuvu
Mbeya City   vs JKT Oljoro
Ashanti Utd   vs Rhino
Prisons    vs Mgambo 
Machi 8, 2014
Mbeya City   vs Rhino
R.Shooting   vs JKT Oljoro
Prisons    vs Simba SC 
*************
Machi 8, 2014
Coastal U    vs Ashanti Utd 
Machi 9, 2014
JKTRuvu    vs Mtibwa S 
Machi 12, 2014
Simba SC    vs Coastal
Mgambo     vs  Mtibwa 
Machi 15, 2014
Azam FC    vs Coastal
Mtibwa S    vs Yanga SC
Kagera S    vs Prisons 
*************
Machi 15, 2014
R.Shooting   vs Ashanti Utd 
Machi 16, 2014
JKTRuvu    vs Mbeya City 
Machi 19, 2014
Yanga SC    vs Azam FC
Mbeya City   vs Prisons 
Machi 23,2014
Ashanti Utd   vs JKT Oljoro
Kagera S    vs R.Shooting
Mtibwa S    vs Coastal U 
**************
Machi 23, 2014
JKTRuvu    vs Rhino
Kagera S    vs R.Shooting 
March 26, 2014
Azam FC    vs Simba SC 
March 26, 2014
Mgambo     vs  Yanga SC 
March 30, 2014
Coastal U    vs Mgambo
JKT Oljoro   vs Prisons
Rhino     vs  Mtibwa S 
***************
Machi 30, 2014
Ashanti Utd   vs Mbeya City 
Aprili 2, 2014
R.Shooting   vs Azam FC
Yanga SC    vs JKTRuvu 
Aprili 6, 2014
Mgambo     vs  Azam FC
Rhino     vs  Yanga SC
Mtibwa S    vs R.Shooting 
Aprili 9, 2014
Yanga SC    vs Kagera S 

***************
Aprili 9, 2014
Azam FC    vs JKT Oljoro
Coastal U    vs JKTRuvu 
Aprili 12, 2014
Mgambo     vs  Kagera
Prisons    vs Rhino 
Aprili 13, 2014
Simba SC    vs Ashanti Utd 
Aprili 23, 2014
Mbeya City   vs Azam FC
JKT Oljoro   vs Yanga SC 
***************
Aprili 27, 2014
Rhino     vs  R.Shooting
Mbeya City   vs Mgambo
Prisons    vs Ashanti Utd
JKTRuvu    vs Azam FC
JKT Oljoro   vs Mtibwa
Coastal U    vs Kagera
Yanga SC    vs Simba SC 
***************

Waziri anusurika Kifo ajali ya ndege

* Ndege iliserereka na kuingia vichakani
Waziri Abubakar Khamis Bakar aliyenusurika kifo katika ajali ya ndege jana Zanzibar

Na Suleiman Rashid Omar Pemba

WAZIRI wa Katiba na Sheria Zanzibar, Abubakari Khamis Bakari, pamoja na abiria 17 wamenusurika kifo, baada ya ndege ya shirika la ndege la ‘Zan air’ waliyokuwa wanasafiria kupata matatizo ya breki na kusererekea vichakani.
Ndege hiyo iliyokuwa na marubani wawili, iliserereka wakati inatua katika uwanja wa ndege wa Karume kisiwani Pemba ikitokea Unguja juzi jioni.
Kamanda wa Polisi Mkoa Kusini Pemba, Swalehe Mohamed Swaleh, akizungumzia ajali hiyo alisema ilitokea  baada ya ndege hiyo kuwasili Pemba ikitokea Unguja.
Alieleza kuwa ilikwenda kwa kasi kama kawaida ikitarajiwa kuwa ingepunguza mwendo lakini ilishindwa kufanya hivyo.
“Ni kweli ndege hiyo ya ‘Zan Air’ ilipata hitilafu na kuingia majanini lakini abiria wote waliokuwamo na marubani wawili, walitoka salama,’’alifafanua.
Alisema polisi imeliimarisha ulinzi wa ndege  na abiria hao na haikuruhusiwa watu wasiohusika kuzengea eneo hilo.
Baadhi ya mashuhuda  walioishuhudia ndege hiyo walisema ilikwenda kwa kasi kubwa kama gari zinazofukuzana na kumfanya muongoza ndege uwanjani hapo kukaa pembeni akishangazwa na kilichotokea.
Walisema baada ya kuiona ikiwa haipunguzi mwendo kasi kama inavyotakiwa, ghafla iliingia majanini na kuacha barabara ya ndege.
Mkuu wa kikosi cha zima moto na uokozi kisiwani Pemba Shaban Zidi Heri Juma, alishuhudia  ndege hiyo ikikimbia kwa kasi kubwa ambapo gari la zima moto liliifuata kwa haraka hadi iliposimama kichakani.
 Meneja wa uwanja huo,  Rajabu Ali Mussa, alisema tukio hilo lilitokea saa 10:30 jioni jana na kwamba ilipata hitilafu baada ya uchunguuzi wa awali kuonyesha matatizo ya breki.
Alifafanua kuwa  wataalamu watachunguza ili kujua chanzo cha hitilafu kwenye breki.
NIPASHE