STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, July 30, 2012

Ubalozi wa UAE kutumia zaidi ya Dola 1200,000 kufuturisha mikoa saba nchini

UBALOZI wa Nchi za Falme za Kiarabu (UAE) nchini, kupitia taasisi za Sheikh Khalifa bin Zayed Al Hahyan, Sharjah Charity Internation na Red Cresent, unatarajia kutumia zaidi ya dola 120,000 za Marekani, kuifadhili mikoa saba nchini kwa ajili ya futari na Zakatul Fitr kipindi chote cha mfungo wa mwezi wa Ramadhani. Akizungumza kwa niaba ya Balozi wa UAE nchini Tanzania, Mallalla Mubarak Al Ameir na msaidizi wake, Mohammed Obaid Salem AlZaabi, baada ya kugawa futari katika msikiti wa Al Makbool, Msasani Dar es Salaam juzi, Mhasibu wa ubalozi huo, Abdallah Ahmedina, alisema baadhi ya msikiti ya mikoa hiyo ndiyo itakayonufaika. Ahmedina, aliitaja mikoa ambayo waumini wake tangu kuanza kwa mfungo wa mwezi wa ramadhani wamekuwa wakifuturishwa na watakuja kupewa Zaka kwa ajili ya Eid El Fitri ni Dar es Salaam, Iringa, Kilimanjaro, Arusha, Pwani, Dodoma na Morogoro. Mhasibu huyo alichangua kuwa kiasi cha dola 80,000 zinatoka asasi ya Khalifa, dola 36,000 kutoka Red Cresent na dola 6,000 zinatoka Sharjah na kusema utaratibu huo wa kusaidia waumini wa misikiti ya mikoa hiyo umeanza tangu ubalozi wao uwe nchini na utaendelea kwa lengo la kuwasaidia waumini kutekeleza ibada yao ya funga bila ya hofu ya kukosa futari au kuisherehea Eid. Alifafanua, kati ya fedha hizo zilizotolewa na asasi hizo tatu zinatumika kwa futari na zilizosalia ni kwa ajili ya kugawa Zakatul fitr ambayo huwalenga waumini wajane, yatima, walemavu, maskini na fukara ili kuisherekea sikukuu kwa furaha na amani. "Miaka yote huwa tunatoa futari na kugawa zakatufitr, mwaka huu tutatumia kama dola 122,000 za Marekani zinazotolewa na asasi zilizopo chini ya ubalozi wetu za Sheikh Khalifa, Red Cresent na Sharjah Charity," alisema. Akitoa shukrani kwa niaba ya waumini wake, Imamu wa msikiti wa Al Makbool, Sheikh Mussa Abdallah, aliushukuru ubalozi huo kwa kile walichosema umewasaidia kutimiza moja ya nguzo za dini yao. "Waumini wengine hawana uwezo wa kupata futari kama hii, tunashukuru ubalozi na asasi zote zilizochangia msaada huu na Inshallah, Mwenyenzi Mungu awazidishie," alisema Imamu Abdallah. Alisema baadhi ya watu waliokuwa hawafungi kwa kutokuwa na hakika ya kupata futari kwa sasa hawana sababu tena kwa vile wamepata uhakika wa kupitia ufadhili huo wa ubalozi wa UAE.

No comments:

Post a Comment