STRIKA
USILIKOSE
Wednesday, August 8, 2012
Azam yazidi kung'ang'ania Redondo yaionya Simba
WAKATI kiungo Ramadhani Chombo 'Redondo' akisisitiza kuwa, hana mkataba na klabu ya Azam na ndio maana ameamua kusaini kuichezea Simba, uongozi wa klabu ya Azam umeendelea kushikilia msimamo kwamba kiungo huyo ni mali yao na Simba 'imeliwa'.
Katibu Mkuu wa Azam, Idrissa Nassor alisema wao sio wehu wakurupuke kung'ang'ania kwamba Redondo ni mali yao iwapo hawana mkataba nae na kudai Simba wanajisumbua na kuweza kuwakuta kama lililowakuta kwa mchezaji Ibrahim Juma 'Jebba' waliokuwa wakimng'ang'ania kutaka kumsajili.
Nassor ambaye ni maarufu kwa jina la 'Father' alisema, Redondo ni mali yao kwa vile wana mkataba utakaomalizika mwakani mwezi Juni, na hivyo Simba kama wanamhitaji kiungo huyo ni wajibu wa kuzungumza nao ili wawape kwa utaratibu unaotakiwa.
"Sio sio wajinga kumng'ang'ania Redondo, pia hatuwezi kumzuia iwapo anataka kwenda Simba, ila taratibu zinatakiwa kufuatwa kwa vile tunaye mkataba nae unaomalizika Juni mwaka 2013," alisema Nassor.
Alisema kinachoendelea kwa Simba na Redondo hakutofautiani na sakata la Jebba ambaye Simba ilidai kumsajili na kwenda nae kwenye michuano ya Ujirani Mwema kabla ya kubaini kwamba walikuwa wakijisumbua kutokana na ukweli mchezaji huyo alikuwa na mkataba na Azam.
Hata hivyo Redondo akizungumza na vyombo vya habari jana, alisema yeye hana mkataba na Azam kwa vile mkataka wake wa awali ulishaisha tangu Juni mwaka huu, pia akisema kilichomfanya aondoke ni kutoitwa na viongozi kupewa mkataba mpya.
Pia alisema 'kifungo' cha miezi minne alichopewa na uongozi wa Azam kwa tuhuma za utovu wa nidhamu ni sababu nyingine iliyomfanya 'aipe' kisogo timu hiyo na kutua Simba ambayo aliichezea kabla ya kutua Azam misimu miwili iliyopita.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment