STRIKA
USILIKOSE
Saturday, August 11, 2012
TAFF, Bongo Movie, wasambazaji waungana kudhibiti wezi
MAKAMPUNI ya usambazaji wa kazi za wasanii kwa kushirikiana na Shirikisho la Filamu
Tanzania, TAFF na Mamlaka ya Mapato Tanzania, TRA, wameungana pamoja na kutangaza
'vita' dhidi ya maharamia na wezi wa kazi za wasanii kwa lengo la kukomesha vitendo hivyo.
Wasambazaji hao, Steps Entertainment, PAPAZI, Msama Promotions na wengine wameamua
kushirikiana na TRA, Bongo Movie na TAFF kwa nia ya kukomesha vitendo hivyo sawia na
kulinda masilahi ya wasanii ambao wamenyonywa kwa muda mrefu.
Wakizungumza katika mkutano uliofanyika jana jijini Dar es Salaam
viongozi wa 'umoja' huo walisema umefika wakati wa kukomesha tatizo hilo la muda mrefu ambalo limekuwa likiwakatisha tamaa wadau wa sanaa nchini.
Rais wa TAFF, Simon Mwakifwamba, alisema wameona hakuna njia ya kukomesha hilo kama sio kufanya kazi kwa pamoja katika kulishughulikia akidai anashangazwa na kukithiri kwa hali hiyo ilihali kuna sheria juu ya udhibiti wa jambo hilo.
Alisema, mbali na muunganiko wao, pia wanaiomba serikali kutekeleza ahadi yake ya kuwasaidia wasanii kupambana na maharamia, aliodai wapo kila pembe ya nchi hii wakifanya uhalifu wao kwa kujiamini kana kwamba wapo juu ya sheria.
Mwakifwamba aliongeza kwa kusema lau kazi za wasanii zitasimamiwa vizuri, zitaliongezea taifa pato kubwa kw avile soko la sanaa kwa sasa limekuwa na mafanikio makubwa ingawa bado inawanufaisha wachache.
Naye Mwenyekiti wa Bongo Movie, Jacob Steven 'JB' alisema sanaa inaweza kuwa na nafasi ya tatu kwa kuchangia pato la taifa ukiacha pato linalotokana na sekta za madini, maliasili na utalii.
Kwa upande wa TRA, Meneja Usimamizi, Msafiri Ndimbo alisema Mamlaka hiyo imejipanga
kudhibiti wizi wa kazi hizo kuanzia Januari mwakani baada ya serikali kupitia Bunge lake kukubalina kuweka mikakati ya kupamba na suala hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment