STRIKA
USILIKOSE
Sunday, August 12, 2012
Ruvu Shooting yatangaza kikosi chake kipya, yasajili 26
KLABU ya soka ya Ruvu Shooting Stars inayojiandaa na Ligi Kuu Tanzania Bara imetangaza usajili wa wachezaji wao 26 kwa ajili ya msimu mpya wa ligi hiyo utakaoanza mwezi ujao.
Miongoni mwa waliosajiliwa na kikosi hicho kinachonolewa na kocha Charles Boniface Mkwasa ni pamoja na waliokuwa washambuliaji nyota wa Kagera Sugar, Hussein Swedi na Said Dilunga.
Msemaji wa klabu hiyo, Masau Bwire aliiambia MICHARAZO leo asubuhi kuwa, usajili huo ambao unatarajiwa kuwasilishwa kesho kwenye ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, umezingatia umri, kipaji na uwezo wa mchezaji kutokana na mapendekezo ya kocha wao.
Bwire, alisema kati ya wachezaji hao 26 waliosajiliwa na klabu yao, sita ni wachezaji wapya na waliosalia ni wale walioichezea timu hiyo msimu uliopita.
Aliwataja wachezaji wapya walionyakuliwa na timu yao kuwa ni Said Dilunga, Husseni Swedi, Mau Bofu aliyekuwa akiichezea Azam, Gideon Sepo, Kulwa Mobi aliyeichezea Polisi Dodoma msimu uliopita na Philemon Mwandesile aliyekuwa timu ya Toto Afrika.
Wachezaji wa zamani waliobakishwa kikosi ni pamoja na kipa Benjamin Haule, Michael Norbert, Gido Chawala, Godhard Msweku, Liberatus Manyasi, George Assey, Mangasin Mbonosi, Paul Ndauka, Jumanne Juma, Shaaban Suzan, Said Madega na Nyambiso Athuman.
Wengine ni Raphael Keyala, Frank Msese, Michael Aidan, Gharib Mussa, Ayuob Kitala, Ernest Jackson na Baraka Nyakamande.
Bwire alisema wachezaji waliotemwa na kikosi hicho kutokana na sababu mbalimbali ni pamoja na Mohammed Kijuso, Emmanuel Mwagamwaga, Yusuph Mgwao na Kassim Kilungo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment