Mwita, Naali vinara Rock City Marathon 2012
Mwanariatha Mary Naaly kutoka Arusha akishangilia baada ya kumaliza
mbio za kilometa 21 na kuibuka mshindi kwa upande wa wanawake katika
mashindano yanayojulikana kama ‘Rock City Marathon 2012’ yaliyofanyika
Jijini Mwanza jana Jumapili. Naaly alizawadiwa shilingi 1,200,000/= ya
ushindi baada ya kutumia saa 1:16:33 kumaliza mbio hizo na kuwashinda
wenzake zaidi ya 497 walijitokeza kushiriki mashindano hayo.
Mwanariatha Copro Mwita kutoka Mwanza akishangilia baada ya kumaliza

mashindano yanayojulikana kama ‘Rock
City Marathon 2012’ yaliyofanyika Jijini Mwanza jana Jumapili. Mwita
alizawadiwa shilingi 1,200,000/= ya ushindi baada ya kutumia saa 1:04:02
kumaliza mbio hizo na kuwashinda wenzake zaidi ya 375 walijitokeza
kushiriki mashindano hayo.
Wanariadha
walioshiriki mbio za Rock City Marathon 2012 kilometa 21, wakichuana
vikali kutafuta shilingi 1,200,000/= ambayo waandaaji wa mbiyo hizo,
Capital Plus International Ltd (CIP), walitenga kwa mshindi wa mwaka
huu. Mashindano hayo yalifanyika Mwanza.

huu. Mashindano hayo yalifanyika Mwanza
MWANZA, Tanzania
MWANARIADHA
mahiri Copiro Mwita wa Mwanza na Mary Naaly wa Arusha, jana waliibuka
vinara upande wa wanaume na wanawake, katika mashindano ya riadha ya
kilometa 21 ya ‘Rock City Marathon 2012’ yaliyofanyika leo Jijini
Mwanza.
Mwita
alishinda mbio hizo kwa upande wa wanaume akitumia saa 1:04:02, huku
Mary akishinda kwa upande wa wanawake baada ya kutumia saa 1:16:33,
katika mashindano hayo yaliyoshirikisha zaidi ya wanariadha 497
waliokimbia katika makundi matano.
Dotto Ikangaa
kutoka Arusha aliibuka mshindi katika mbio za kilometa tano wanaume,
akimpiku John Joseph kutoka Singida ambaye alishika nafasi ya pili, huku
Paul Elias kutota Ukerewe, Mwanza akishika nafasi ya tatu.
Rock City
Marathon ni mbio zinazondaliwa na kampuni ya Capital Plus International
Ltd tangu mwaka 2009, ambapo kwa mwaka huu zilidhaminiwa na NSSF, Airtel
Tanzania, Geita Gold Mine, ATCL, PPF, African Barrick Gold, New Africa
Hotel, Nyanza Bottles, New Mwanza Hotel, TANAPA na Bodi ya Utalii
Tanzania (TTB).
Katika mbio
hizo, washiriki na mashabiki wake waliburudishwa na msanii maarufu wa
Tanzania Juma Kassim ‘Sir Nature’ na kundi lake la TMK Wanaume,
akishirikiana na Baby Madaha katika kuuzindua wimbo wao mpya ‘Narudi
Nyumbani’ ambao waliimba kwa mara ya kwanza Mwanza.
Rais wa
Shirikisho cha Riadha Tanzania (RT), Anthony Mtaka, ambaye alikuwa ni
mgeni rasmi, licha ya kutoa onyo kwa wavamizi wa viwanja vya michezo,
alionesha kuridhishwa nuratibu wa Rock City Marathon, huku akiongeza
kuwa mbio hizi zimeweza kuibua vipaji vingi vya riadha ambayo vinahitaji
kukuzwa.
“Nawashukuru
sana waandaaji wa Rock City Marathon kwa kuweza kuandaa mashindano
ambayo yameweza kutusaidia sisi wadau wa riadha kugundua vipaji vingi
ambavyo tunavyo hapa nchini ambavyo vinahitaji kukuzwa,” alisema Mtaka
ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Morogoro.
“Hivyo basi
natoa wito kwa makampuni, mashirika na hata serikali, kuweza kudhamini
mashindano kama haya ambayo yanasaidia sana kuendeleza na kuibua vipaji
vya mchezo wa riadha ambao umeliletea sifa kubwa taifa letu huko nyuma,”
alisisitiza Mtaka.
Kwa upande
wake, Katibu Mkuu wa RT, Suleiman Nyambui alisema Rock City Marathon
imeonesha kuvuta hisia na kukubalika miongoni mwa washiriki, kutokana na
kuhusisha mbio za ngazi zote; nusu marathon, kilometa tano, kilometa
tatu kwa walemavu, kilometa tatu kwa wazee na kilometa mbili kwa watoto.
Washiriki
kutoka mikoa mbali mbali nchini walishiriki Rock City Marathon 2012,
pamoja na wageni kutoka nchi za India, Canada, Australia, Afrika Kusini,
Rwanda, Kenya na Uganda, ambapo washindi wa pili wa mbio za kilometa
21, wanaume na wanawake walijishindia shilingi 900,000 kila mmoja.
Washindi wa
tatu kilometa 21 waliondoka na shilingi 700,000 kila mmoja na wa nne
hadi wa 10 walizawadiwa shilingi 150,000 kila mmoja. Wale walioshika
nafasi ya 11 hadi 25 waliondoka na kifuta jasho cha shilingi 100,000
kila mmoja kwa upane wa wanaume na wanawake.
Jeremiah
Kinshuzi wa Mwanza alishinda mbio za kilometa tatu kwa wazee, huku
Pascal Emanuel wa Kisese akishinda kwa watu wenye ulemavu na
walizawadiwa shilingi 50,000 kila mmoja, shilingi 30,000 kwa washindi wa
pili na washindi wa tatu wakijipatia shilingi 20,000.
Kwa upande wa
watoto ambao walikimbia kilometa mbili, Idd Suguta wa Mara na Emma
Imhoff wa Singida waliibuka washindi na kuzawadiwa shilingi 30,000 kila
mmoja, huku washindi wa pili wakipata shilingi 20,000 na wa tatu 15,000
na walioshika nafasi ya nne hadi 25 wakapata kifuta jasho cha shilingi
10,000 kila mmoja.
source:
SOURCE: francisdande.blogspot.com

No comments:
Post a Comment