UMEWAHI KUMUONA ALIYETUNGA JINA LA TANZANIA? HUYU HAPA..
Kiongozi wa Ahmadiya Nchini Tahir Mohamedi,akitoa neno baada ya Uzinduzi wa msikiti huo |
Waumini wa kiislam wa mjini Lindi wakishuhudia tukio hilo. |
Waumini wa kiislam wa mjini Lindi wakishuhudia tukio hilo |
Mssikiti uliozinduliwa unavyoonekana. |
Rai hiyo imetolewa jana na mwanzilishi wa jina la Taifa hili (Tanzania) Mohamedi Igbal Dar,alipokuwa anazungumza na timu ya waandishi wa habari hizi muda mfupi baada ya kikao cha ndani cha
ufunguzi wa Misikiti uliojengwa mjini Lindi,kwa ufadhili wa Taasisi ya Ahmmady Iqbal, alisema vitendo vya vurugu vinayoanza kushamili hivi sasa hapa nchini, visipoangaliwa kwa umakini na kuchukuliwa hatua,vinaweza kulipeleka taifa kwenye machafuko yasiyoisha, na hivyo kuondoa sifa ya Tanzania aliyoiacha mwanzishi wa taifa hili, mwalimu Nyerere miaka kumi na tatu iliyopita.
Alisema kuwa vurugu zinazojitokeza hivi sasa kwenye Shughuli mbalimbali zikiwemo za dini pamoja na siasa, ni ishara mbaya kwa nchi kama ya Tanzania,ambayo imetimiza zaidi ya miaka 50 ya uhuru wake,na
kugeuzwa kuwa ni kisiwa cha amani na utulivu.
Igbal ambaye kwa sasa maisha yake yapo nchini Uingereza, alisema kuna haja ya vitendo hivyo kudhibitiwa mapema iwezekanavyo kabla havijaota mizizi ya kuatarisha amani, umoja na mshikamano uliopo wa taifa hili.
Alisema kwamba vurugu sio jambo la kujivunia sana katika Taifa linahitaji kuendelea, kama la Tanzania na kuwasisitiza watu wasiojua athari za kivita vya kidini waangalie nchi za jirani kama vile
Somalia ambapo wananchi wake wanaishi bila amani..
Nae kiongozi wa Jumuia ya Ahmmadyya nchini Tanzania Tahir Mohamedi, amewataka waislamu kufuata sheria kanuni na makatazo ya mwenyezimungu kupitia kwa Mtume wake Muhammad (Saw) kuungana na kuwa kitu kimoja kwa kuwa dini yao, haifundishi waumini wake kueneza chuki.
Tahir alisema dini zote dunia zinafundisha amani, huruma na upendo miongoni mwa waumini wake watu wengine, lakini ikiwa watu wachache wanaenda kinyume na maagizo ya mungu basi sio vizuri jamii
kuwahukumu waislamu wote wa Tanzania.
“Unajua mwanzilishi wa Jumuhia ya waislamu wa Ahmmadyya ametufundisha kuwa ikiwa mnapenda kupata ridhaa ya mungu basi takaseni mioyo yenu kwa kuwa haina wazo la chuki na fanyeni
uadilifu hata kama mbele yenu kuna adui yenu” alisema Tahir
No comments:
Post a Comment