MCHEKESHAJI mahiri ambaye pia ni msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Hussein Mkiety ‘Sharo Milionea’amefariki
papo hapo usiku wa kuamkia leo baada ya kupatwa ajali akielekea nyumbani kwao Muheza, mkoani Tanga.
.
Msanii Husseni Mkiety 'Sharo Milionea' enzi za uhai wake |
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Tanga, Constantine Massawe alinukuliwa na kituo kimoja cha redio na kuthibutisha taariofa za kifo cha msanii huyo machachari.
“Leo majira ya saa mbili usiku kwenye barabara ya Segera Muheza Tanga mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Hussein Ramadhani au Sharo Milionea akiwa anaendesha gari namba T478 BVR Toyota Harrier akitokea Dar es salaam kwenda Muheza alipofika eneo hilo gari lake liliacha njia na kupinduka mara kadhaa na kusababisha kifo chake.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali Teule ya wilaya ya Muheza” Kamanda amesema hakuna kona kali sana wala ubovu wa barabara kwenye sehemu aliyopata ajali Sharo Milionea, katikati ya Segera na Muheza ambapo gari imehifadhiwa mahali salama kwa sababu haitembei.
Taarifa hii imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa Tanga Constantine Massawe,
Hadi mauti inamkuta alikuwa ni mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya wimbo wake wa Chuki Bure alioimba na Dully Sykes mbali na kibao chake cha 'Hawataki'.
taarifa zaidi kuhusu taratibu za mazishi tutaendelea kuwajulisha
ingawa inaelezwa msiba wake upo nyumbani kwao Muheza Tanga.
Mola airehemu roho yake mcheshi Sharo Milionea.Tulimpenda sana huku Kenya kwa ujasiri wake mkumbwa.Kifo hakina huruma kweli
ReplyDelete