MTANGAZAJI ALIYEPOTEA AKUTWA PORINI AMEKUFA HANA SEHEMU NYETI
Bw. Issa Ngumba. |
Mwandishi wa habari wa Radio Kwizera anayefanyia kazi wilayani Kakonko mkoani Kigoma,Bw. Issa Ngumba aliyepotea katika mazingira ya kutatanisha amekutwa amekufa huku akiwa kanyofolewa sehemu zake za siri.
Taarifa kutoka Kigoma ambazo mtandao huu MICHARAZO umezipata jana kuwa, mwili
wa mwanahabari huyo umekutwa nje kidogo na mkoa wa Kigoma.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Kigoma Frasser Kishai, amethibitisha juu ya kutokea
kwa tukio hilo na kwamba bado jeshi la polisi linaendelea kufanya uchunguzi.
Mbunge wa jimbo la Kigoma Zitto Kabwe amenukuliwa kusikitishwa na kifo cha mwandishi huyo na kulitaka jeshi hilo kufanya uchunguzi wa kina juu ya kifo chake.
Kabwe ameeleza jinsi mwanahabari huyo alivyokuwa akiifanya kazi yake kwa jamii ya Kigoma kwa ufanisi zaidi na kuwa wakati
mwingine yeye kama mbunge alikuwa akizunguka na mwanahabari huyo katika
jimbo lake.
" Kweli nimeguswa sana na kifo cha kusikitisha cha mwanahabari huyo
nilimfahamu vema kwa utendaji kazi wake ila nawapa pole sana
waandishi wote nchini kwa msiba huu mkubwa .....na zaidi nitapata
kueleza mengi mara baada ya uchunguzi"
Taarifa za awali
zilizotolewa na Jeshi la Polisi wilayani Kakonko baada ya kupotea kwa
mwanahabari huyo zilisema kuwa Bw Ngumba alipotea tangu
January 05 mwaka huu majira ya saa 11 jioni ambapo alimuaga mke wake Bi.
Rukia
Yunus kuwa anakwenda Muhange senta wilayani Kakonko na kwamba hajarudi
nyumbani hadi sasa.
Kufuatia
tukio hilo jeshi la polisi kwa kushirikiana na wananchi wa Kijiji cha Muhange
wanaendelea kumtafuta katika mapori ya kijiji hicho baada ya rafiki zake
kueleza kuwa aliwaanga kuwa anakwenda kutafuta dawa msituni.
Bw. Issa Ngumba. |
Aidha jeshi
la polisi Wilayani Kibondo liliomba kampuni za mitandao ya simu anayotumia Bw
Ngumba kusaidia kutambua simu zake zilipotumika kwa mara ya mwisho ili
kurahisisha upatikanaji wake.
CHANZO:FRANCIS Godwin
No comments:
Post a Comment