STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, January 23, 2013

Simba yamalizana na akina Ochieng

Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji iliyokutana Januari 19 mwaka huu chini ya Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa, imeliondoa shauri lililokuwa mbele yake dhidi ya klabu ya Simba lililowasilishwa na wachezaji Pascal Ochieng na Daniel Akuffor baada ya pande hizo kufikia makubaliano.
Wachezaji hao kutoka Kenya na Uganda waliwasilisha malalamiko mbele ya kamati wakipinga kukatizwa mikataba yao bila kulipwa stahili zao. Hata hivyo, pande zimefikia makubaliano ya kuvunja mikataba nje ya kamati, na wachezaji hao kulipwa stahili zao.
Simba imekiri vilevile kudaiwa na wachezaji Shija Mkina, Swalehe Kabali, Victor Costa na Rajab Isiaka na kuahidi kuwalipa wachezaji hao wakati Coastal Union na mchezaji wake Mohamed Issa wamefikia makubaliano ya malipo, hivyo kuvunja mkataba kati ya pande hizo mbili.

Wakati huo huo kikosi cha timu hiyo ya Simba kilichokuwa Umangani kinatarajiwa kutua leo na kesho kikitarajiwa kushuka dimba la Taifa, Dar es Salaam kuvaana na Black Leopards ya Afrika Kusini.
Simba na Loepards watapambana katika mechi ya kirafiki ya kimataifa, ikitarajiwa kutambulisha mbinu walizojifunza wakiwa Oman.
Black Leopards leo wanatarajiwa kuvaana na Yanga katika pambano la marudiano litakalofanyika jijini Mwanza.
Pascal Ochieng
Katika mechi yao ya awali Yanga iliwalaza Waafrika Kusini haoa mabao 3-2, jijini Dar na pambano hilo la leo linatarajiwa kuwa na upinzani kila upande ukitamba kufanya kweli.

No comments:

Post a Comment