STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, February 23, 2013

Balotelli katika vita vya mahasimu wa jiji la Milan leo



MILAN, Italia
AC Milan iliyomaliza mwenendo mbaya katika Ligi Kuu ya Seria A, leo inatarajiwa kushuka dimbani kukabiliana na wapinzani wao wakuu, Inter Milan, ikimtegemea 'mtukutu' Mario Balotelli.

Balotelli aliyeifungia Ac Milan mabao manne katika mechi tatu alizoichezea katika ligi na kuifanya iikaribie vinara Juvetus atashuka dimbani kuikabili timu yake ya zamani.
bovu, ikiwa na furaha ya kuifunga Barcelona, inakutana na Inter Milan iliyo katika janga la katikati ya msimu katika mechi ya mahasimu wa Serie A kesho ambayo pia itahusisha mshambuliaji mwenye vituko Mario Balotelli kuikabili klabu yake ya zamani.
'Super Mario' ambaye huwa hatabiriki atakuwa akipambana na klabu ambayo aliichezea kwa misimu minne na kuonekana kwa mara ya kwanza kwenye ngazi ya ligi kuu.
Kocha wa Inter Andrea Stramaccioni ametoka kidedea katika medhi zake zote zilizopita dhidi ya AC Milan na anahitaji kwa gharama yoyote ushindi wa tatu ili kuokoa msimu wa timu yake.
Mahasimu hao wa Milan wamebadili nafasi tangu kuanza kwa mwaka mpya ambapo AC Milan, ambayo kusuasua kwake mwanzoni mwa msimu kulipelekea ubashiri wa kila wiki wa hatma ya kocha Massimiliano Allegri, sasa ipo juu ya Inter.
Milan imekusanya pointi 23 kutoka katika mechi 10 tangu mwanzo wa Desemba na ni ya tatu ikiwa na pointi 44, moja zaidi ya Inter.
Inter imekusanya pointi 15 katika kipindi hicho na imekutana na vipigo vitatu vibaya tangu kuanza kwa msimu, nyumbani kwa Udinese, vibonde Siena na kuchabangwa 4-1 na Fiorentina Jumapili iliyopita.
Kocha wa zamani wa timu za vijana Stramaccioni alipandishwa ngazi kuifundisha Inter msimu uliopita na ushindi wao wa 4-2 dhidi ya Milan ulimaliza matumaini ya mahasimu wao kutwaa ubingwa. Pia ilsihinda mechi ya kwanza msimu huu 1-0.
"Jambo zuri na baya katika kuwa kocha wa Inter ni kuwa shinikizo lipo tangu siku ya kwanza nilipoanza kufundisha timu hii mashuhuri," alisema Stramaccioni.
"Kama kocha katika ngazi hii anafikiri kuhusu mambo haya, basi amekwisha kabla ya kuanza kazi," alisema zaidi mwalimu huyo mwenye miaka 37.

No comments:

Post a Comment