STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, February 23, 2013

Yanga yashtakiwa tena FIFA, uongozi wajitetea


KLABU ya soka ya Yanga, imeingia tena matatani baada ya kuburuzwa katika Shiriksho la Soka Duniani, FIFA na nyota wake wa zamani Mghana Kenneth Asamoah.
Asamoah ameiburza Yanga FIFA ikiidai Dola 5000 za Kimarekani ikiwa sehemu ya malipo yake ya kujiunga na klabu hiyo ambayo iliamua kumtema msimu huu.
FIFA limetoa taarifa ya kulipeleka rasmi madai ya mchezaji huyo kwenye chombo chake cha utatuzi wa migogoro (Dispute Resolution Chamber) baada ya klabu hiyo kutojibu chochote.
Awali FIFA ilipokea malalamiko ya Asamoah kuwa anaidai Yanga dola 5,000 za Marekani ambapo ilikuwa ni sehemu ya malipo yake (signing fee) baada ya kujiunga na klabu hiyo.
Desemba mwaka jana FIFA iliiandikia barua Yanga kupitia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ikitaka maelezo yake kuhusu madai hayo ya Asamoah, lakini hadi sasa haijajibu madai hayo.
Kwa mujibu wa FIFA, hatua ya uchunguzi wa suala hilo umekamilika, na sasa linapelekwa rasmi katika chombo chake cha utatuzi wa migogoro (Dispute Resolution Chamber) kwa ajili ya kufanya uamuzi.
Hilo ni tukio la tatu la hivi karibuni kwa Yanga kufikishwa FIFA awali iliburuzwa na beki wao zamani John Njoroge na kocha Kostadin Papic iliyowavunjia mikataba kabla ya wakati.
Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrance Mwalusako alinukuliwa jana akidai kuwa, uongozi utamlipa fedha hizo Asamoah akisema kabla ya hapo walishapunguza deni alililokuwa akiidai klabu hiyo la karibu Sh Milioni 10.
"Hizi fedha zitalipwa sio kitu cha kukuzwa, uongozi umechelewa kummalizia kwa kuwa ilikuwa ikiendelea na uhakiki wa madeni inayodaiwa klabu, ila tunauhakikishia umma kwamba Asamoah atapewa fedha zake haraka iwezekanavyo,": alisema Mwalusako.
Alisisitiza kuwa, uongozi wao umekuwa ukionekana kama 'wababaishaji' ilihali madeni inayoangaika nayo ni ya uongozi uliopita na kuwataka wanayanga kutulia kwani kila kitu kinaenda vema na uongozi wao upo makini katika kurekebisha dosari zilizopo.

No comments:

Post a Comment