STRIKA
USILIKOSE
Saturday, February 23, 2013
Himid Mao aipa Azam ubingwa wa Tanzania Bara
KIUNGO mkabaji wa klabu ya Azam, Himid Mao ametangaza na kuipa ubingwa klabu yake ya Azam, licha ya kukiri kwamba Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu huu ni ngumu na isiyotabirika haraka.
Mao, mtoto wa nyota wa zamani wa Pamba, Simba, Mtibwa Sugar na Taifa Stars, alisema anaamini kwa kikosi ilichonacho Azam ni dhahiri wanastahili kuwa mabingwa wapya wa Tanzania msimu huu.
Alisema, licha ya kuwepo kwa mchuano mkali katika kuwania taji hilo klabu yake ikibanana na Yanga kileleni na ikifukuziwa kwa nyuma na mabingwa watetezi, bado haoni sababu ya Azam kunyakua taji wakayi ndiyo timu yenye kikosi bora zaidi kwa sasa nchini.
"Ni vigumu kutabiri moja kwa moja bingwa wa msimu huu, lakini kwa kuangalia ubora wa vikosi, Azam ndiyo wanaostahili kuwa Bingwa, na wachezaji tupio tayarai kutimiza ndoto hizo," alisema.
Aliongeza, mbali na kuliota taji la ligi kuu, pia karibu kila mtu ndani ya Azam analipigia hesabu pia kombe la michuano ya Shirikisho Afrika ambapo wiki ijayo Azam watarudiana na El Nasir Juba ya Sudan Kusini mjini Juba katika mechi ya marudiano huku wakiwa na hazina ya ushindi wa mabao 3-1 iliyopata nyumbani.
Mao, aliyeanzia soka la tangu darasa la nne katika Shule ya Dk Omar Juma na kucheza chandimu Kibesa Fc kisha kutua Soccer Rangers zote za Magomeni na baadaye kunyakuliwa na kituo cha Elite Academy kabla ya kusajiliwa na Azam mwaka 2008 akiichezea timu ya vijana ya U20, alisema sababu, uwezo wa Azam kuwa mabingwa wa Afrika kupitia michuano hiyo ya Kombe la Shirikisho inawezekana.
"Tunaomba Mungu atusaidie na kuwaomba Watanzania watuunge mkono, tutimize ndoto hizo za kuwa mabingwa wa Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho," alisema.
Mao aliyetwaa mataji zaidi ya matano tangu aanze kucheza soka la ushindani akiwa na Azam U20 na ile ya wakubwa aliyoanza kuichezea katika duru la pili la msimu wa ligi wa 2008-2009 walipopanda daraja, alisema ushindani wa ligi ulivyo sasa umeondoa ule mfumo wa klabu za Simba na Yanga kuhodhi michuano hiyo.
Mbali na kutwaa Kombe la Uhai mara mbili, Mao pia amenyakua ubingwa wa Kombe la Dunia la Vijana U17 la Copa Coca Cola, Kombe la Mapinduzi mara mbili mfululizo na ile ya Hisani nchini Dr Congo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment