MAJANGILI MATATU YAUAWA MKOANI DODOMA
Mwili wa Mtu anayedhani wa kuwa ni Jangili ukiwa umehalibika baada ya
kuuawa kuchinjwa na kuchomwa moto katika chumba cha kuhifadhia maiti
mvumi Dodoma.
Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma David Misime akiwaonyesha waandishi wa
Habari meno 73 ya tembo yenye thamani ya zaidi 225 mil ambayo ni sawa na
tembo 36 pamoja na Gari aina ya Noah NO T 983 BZJ waliokamata juzi
katika kijiji cha Miganga mvimi wilayani Chamwino Dodoma.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma David Misime akifafanua jambo mbele ya
waandishi wa Habri kuhusu tukio la vifo vya watu watatu wanaodhaniwa
kuwa ni majangili waliouawa na wananchi katika kiji cha miganga Mvumi
Dodoma pembeni ni Gari aina ya Noah No T 983 BZJ walilokuwa wakilitumia
na kuku meno 73 ya Tembo.
Na John Banda, Dodoma
MAJANGILI watatu wa nyara za serekali wameuawa kwa mishale yenye sumu na
kisha miili yao kuchomwa moto na wananchi katika purukushani na polisi
walipokuwa wakijaribu kukimbia ili kutorosha meno ya tembo.
Tukio hilo lilitokea jioni ya alhamis wiki hii katika kijiji cha Miganga
kata ya mvumi wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma ambapo miili yao
ilikutwa ikiwa imehalibika kutokana na kuchomwa moto.
Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma David Misime
alisema majangili hayo yaliuawa na wanachi wenye hasira kali kwa zana
mbalimbali za kijadi walipokuwa wanakimbilia polini ili kujiokoa na
mkono wa polisi.
Misime alisema jeshi hilo lipokea taarifa kutoka kwa wananchi wema kuwa
kulikuwa na Gali likitokea Manda likiwa na Meno ya Tembo na kisha
kuweka mtego katika kijiji cha mwitikila ambapo waliona gali aina ya
NOAH T 983 BZJ na kulisimamisha na Dereva wa Gali hilo alifanya kama
anapunguza mwendo na kisha kuondoka kwa mwendo wa kasi.
‘’Polisi wakishirikiana na wananchi walianza kulifukuza walipofika
kijiji cha Miganga Mvumi polisi walifanikiwa kupiga Risasi tairi moja ya
kushoto na hivyo watu watatu waliokuwemo ndani gari hilo waliruka na
kutawanyika, wananchi waliojichukulia sheria mkononi waliwashambulia
kuasi cha kupoteza maisha yao’’, alisema
Aidha kamanda Misime alisema baada ya kulipekua Gari hilo walikutaMeno
73 ya Tembo yenye uzito wa kilo 255.9 yakiwa na thamani ya zaidi ya TSH
225 mil pamoja na hati ya mashitaka [CHARGE SHEET] ambayo ni kesi ya
kuhujumu uchumi namba 4/2012 iliyokuwa imefunguliwa katika mahama yam
panda mkoa wa katavi na Leseni ya Udereva na 4000692535 Aboubakar Peter
huku wakihisi ni mmoja ya waliouawa.
Alisema walikuwa wameshitakiwa kwa kosa la kupatikana na Meno 3 ya Tembo
Tarehe 17.06.2012 na maafisa wanyama poli katika eneo la Msaginya
Wilaya ya Mlele mkoa wa katavi majina ya walikuwa wameshatakiwa ni
Joseph Marius [NGONDO] 59 mkazi wa maili mbili Dodoma, Aboubakar Mhina
25 mkazi wa Mkuhungu Dodoma, Msafiri Milawa 36 mkazi wa Nkuhungu Dodoma
na Petro Mtipula 55 mkazi wa mpanda.
Kamanda alitoa wito kwa wananchi wasijichukulie Sheria mikononi kwani
kwa kufanya hivyo ni kupoteza ushahidi na inawawia vigumu polisi kupata
mtandao inayohusika na matukio kama hayo.
CHANZO:BOSS NGASA
No comments:
Post a Comment