Na Boniface Wambura
LIGI ya Mabingwa wa Mikoa kutafuta timu tatu zitakazopanda kucheza Ligi
Daraja la Kwanza (FDL) msimu ujao chini ya usimamizi wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) itaanza Mei 12 mwaka huu.
Mwisho
wa mikoa kuwasilisha majina ya mabingwa wao ni Mei 1 mwaka huu wakati
ratiba ya ligi hiyo itapangwa mbele ya waandishi wa habari Mei 3 mwaka
huu kwenye ofisi za TFF.
Uwasilishaji
wa jina la bingwa wa mkoa unatakiwa kufanyika pamoja na ulipaji ada ya
ushiriki ambayo ni sh. 100,000. Mfumo wa ligi hiyo ni bingwa wa mkoa X
kucheza na bingwa wa mkoa Y nyumbani na ugenini ambapo mshindi ndiye
anayesonga mbele katika hatua inayofuata.
Usajili
wa wachezaji wa timu hizo ni uleule uliofanyika katika hatua ya mkoa na
unatakiwa kuwasilishwa TFF kwa ajili ya uthibitisho. TFF inapenda
kusisitiza kuwa hakuna usajili mpya wa wachezaji kwa ajili ya ligi hiyo.
No comments:
Post a Comment