Katibu wa RT, Seleman Nyambui |
WANARIADHA Faustine Mussa na Joseph Daudi wa mbio ndefu za marathon wamefuzu kushiriki mashindano ya riadha ya dunia yatakayofanyika Agosti 10 hadi 18 jijini Moscow, Urusi.
Katika mashindano hayo yanayoshirikisha wanariadha wanawake na wanaume kutoka nchi mbalimbali duniani, Tanzania inatarajiwa kupeleka wanariadha zaidi ya watatu endapo watafikia viwango vinavyotakiwa katika mashindano hayo.
Akizungumza juzi Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha (RT), Suleiman Nyambui, alisema wanariadha hao wamefuzu kutokana na viwango walivyoonyesha wakati wakiwania kushiriki michezo ya Olimpiki.
"Tayari tuna uhakika wa kuwa na wanariadha wawili wenye sifa ya kushiriki katika mashindano ya dunia kwa mbio za marathon... sasa bado tunasubiri kupata washiriki watakaofuzu kwa mbio za mita 5,000 na 10,000," alisema Nyambui.
Aliwataja wanariadha wanawake ambao RT inatarajia kuwa watafikia viwango vya kufuzu kwa michuano ya dunia kuwa ni pamoja na Zakia Mrisho (mita 5,000), Sara Ramadhan, Jacqueline Sakilu na Mary Naal wanaokimbia mita 10,000
No comments:
Post a Comment