Miss Tabata 2012 Noela Michael
|
Mratibu wa shindano hilo
Joseph Kapinga amesema kuwa shindano hilo litakuwa ni ya aina yake kulinganisha
na mashindano ya miaka ya nyuma kwani mwaka huu wamemejitokeza warembo wazuri
zaidi.
“Warembo wazuri wamejitokeza
zaidi kuliko mashindano ya tuliyowahi kuyafanya nyuma. Tutakuwa na burudani nyingi
kutoka nje na ndani ya nchi,” alisema mratibu huyo wa Bob Entertainment na Keen
Arts.
Warembo watakaoshiriki kwenye
shindano wanaendelea na mazoezi kila siku katika ukumbi wa Da’ West Park.
Warembo hao ni Pendo
Judica Moshi (20), Madgalena Bhoke (21), Kabula Juma Kibogoti (20), Queen Eliakim
Masha (19), Upendo Dickson Lema (22), Martha
Gewe (19), Zilpha Christopher (19), Hidaya David (22), Aneth Ndumbalo (19),
Amina Ally (18), Dorice Mollel (22), Eunice Nkoha (19), Kazunde Kitereja
(19), Angela Fradius (19), Domina Soka
(21), Rehema Kihinja (20), Glory Jigge (18) na Sophia Claud (21).
Wengine ni Lilian Mpakani
(19), Lilian Msanchu (19), Rita Frank (20), Pasilida Mandali (21), Rafhel Mussa
(19), Jasmin Damian (18), Angelina Mkinga (19), Mercy Mwakasungu (20), Tunu
Hamis (19), Brath Chambia (23), Ray Issa (22), Shamim Abass (22) na Shan Abass
(22).
Kapinga aliwaomba warembo
wenye sifa kuendelea kujitokeza ili waweze kupata wawakilishi bora katika
shindano la Kanda ya Ilala.
"Bado milango iko wazi,
mrembo yoyote anayejiamini kwamba ana vigezo anakaribishwa. Tunataka shindano
la mwaka huu liwe na ushindani zaidi,” mratibu huyo aliongeza.
Warembo 10 watachaguliwa
kushiriki mashindano ya Miss Ilala na baadaye Miss Tanzania.
Anayeshikilia taji la Miss
Tabata kwa sasa Noela Michael ambaye pia ni Miss Ilala.
Waliyojitokeza kudhamini
shindano hilo ni Fredito Entertainment, CXC Africa, Brake Point na Saluti5.
No comments:
Post a Comment